Dr. Ntuyabaliwe Foundation yakabidhi Library!

Naamini wengi mtakuwa mmesikia kuhusu hii giving back to community foundation ambayo inakwenda kwa jina la “Dr Ntuyabaliwe”. Kama hujawahi kusikia habari hiyo basi huu ni mfuko ulio anzishwa na Jacqueline Mengi kumuhenzi baba yake mzazi ambaye alikuwa medical Dr I believe alikuwa Gynecologist  (please kama nimekosea unaruhusiwa kunisahihisha) lakini naamini alikuwa Gynecologist. Anyway, Jacqueline amekuwa anasaidia mambo mbali mbali kwenye jamii kwa kutumia mfuko huu.  Amekuwa akitoa vifaa vya hospitali (incubator)  vya kutunzia watoto ambao wanazaliwa premature / njiti, madawati ya shule na vifaa mbalimbali vinavyotumika mashuleni. Wiki iliyopita alikabidhi Maktaba / Library kwa shule ya awali ya Makumbusho iliyopo jijini Dar es salaam. Na hii ilikuwa mara ya pili kwa Jacqueline kujenga library kwa shule kwa kutumia mfuko huu wenye jina la baba yake. Kama picha inavyo jieleza hapo ilikuwa wanakabidhi library ya kwanza. Hongera sanaaaaaa Jacqueline, such an inspirational. Kama unafatilia hii blog basi utakumbuka huko nyuma niliwahi kusema kuwa sasahivi Jacqueline yupo kwenye “public eyes”  hivyo jamii itapata nafasi ya kumjua Jacqueline ni nani haswa ( her character) and I have to  admit the more I look at her the more I love her! Just lovely and beautiful. Haya na Molocaho hiyo inakwenda Dubai kwa maonyesho. Mungu akisema Yes hakuna wa kukuzuia! You go girl! Hongera Sanaaaaaa ??

Leave a Reply