Mama Keagan: Asante Mungu

Regrann from @nikypal8585 - Asante Mungu wewe ndio uliyenipa huyu mtoto keagan P .Makonda ? wewe ndio mtendaji na msemaji wa mwisho.Umefanya kwa wakati ulio ona ni sahihi ???? umenipa mtoto wangu Keagan najua ulikuwa na sababu kwanini haikutokea wakati nilipotaka mimi. Mimi ni ushuhuda kamili katika maisha ya kila mwanamke au msichana aliyekata tamaa. Usiogope kaa kimya jipe moyo tamka hili neno moyoni mwako MIMI NI USHUHUDA ULIOKAMILI SITA TETEREKA KAMWE MUNGU NITENDEE JAMBO LANGU KWA WAKATI ULIOSAHIHI NA ULIO UPANGA WEWE AMEN??????? -  
Asante Mungu kwa ajili ya mume wangu Paul (Baba keagan)hakika wewe ni jeshi lisilo tetereka kwani imani yako imepimwa kwa njia tofauti ila ulisimama imara??kwa machozi ya kishujaa,ulinitia moyo sana ukuchoka kusema mke wangu wakati wa Bwana huwa ni sahihi pangusa machozi mshukuru Mungu kwani alikuwa amekuandalia faraja ya kudumu.Hakika nimemwona Mungu kila wakati nilipo pata jaribu nilijifunza kukaa kimya na kujipa moyo wa ushujaa na kusema hakuna mwanadamu anayeweza kukamilisha hii furaha ya mimi kuitwa mama na kupakata mtoto aliyetoka kwenye tumbo langu.Nasema tena na tena upendo wa Mungu kwangu hauna kipimo kwani kanipa kicheko na rafiki wa kudumu .Nawapenda wanangu #PK nitawaleanakuwaombea daima ❤️❤️❤️❤️❤️❤️ASANTE MUNGU???? - #regrann

Leave a Reply