“SIMAMA KATIKA NAFASI YAKO, MUNGU ANAMAKUSUDI NA WEWE”

SIMAMA KATIKA NAFASI YAKO, MUNGU ANAMAKUSUDI NA WEWE
Ni wewe pekee mwenye kujua magumu unayoyapitia na uzito wa changamoto unazokumbana nazo katika maisha. Ni wewe pekee mwenye maelazo na lugha sahihi ya kumueleza Mungu juu ya shida zako, usikatishwe tamaa. 

Usinyamazishwe na watu ambao hawajui historia yako, hawajui shida yako, hawajui maumivu yako, na hawajawahi kuyapitia magumu yanayokusonga wala mazingira yako.

Ilikua rahisi watu kumnyamazisha Batimayo kwa sababu walikua hawajui nini maana ya UPOFU

°Usinyamazishwe na watu ambao wana wazazi wao kwa kuwa hawajui nini maana ya kuwa YATIMA

°Usinyamazishwe na watu ambao wako kwenye ndoa zao na hawajui nini maana ya kuachwa/kutelelekezwa, ujane /ugane, au kutalakiwa.

°Usinyamazishwe na wale walio na watoto na hawajui ugumu, maumivu ya kutokuzaa watoto

°Usinyamazishwe na wale walio na wenzi waaminifu na hawajui nini maana ya kusalitiwa.

°Usinyamazishwe na wale walio na kazi na hawajui ugumu wa kutafuta kazi miaka na miaka bila mafanikio.

°Usinyamazishwe na wale walio na watoto waaminifu/wasikivu na hawajui nini maana ya kuwa na watoto wakaidi, waasi, watukutu, walioshindikana.

°Usinyamazishwe na watu ambao wameshafanikiwa kimaisha na hawajui ugumu au shida ya kuwa masikini.

°Usinyamazishwe na wale wenye uwezo wakula Milo mitatu ya maana kwakuwa hawajui nini maana ya kulala na njaa

Wewe ndiye unajua uchungu unaoupitia, maumivu na upweke unajua wewe mwenyewe, kama Batimayo alivyoipaza sauti kwa Yesu, Endelea kuita na Yesu atakusikia hakika!

Nakutia moyo ya kwamba Mungu Yehova Yupo yeye aonae yupo, mwenye usemi wa mwisho juu ya maisha yako ni yeye!

USIOGOPE Yeye sio kipofu hata asione machozi yako, yeye sio kiziwi asisikie maombi yako, na hajakaa kimya kwa maumivu yako, Anajua, Anaona , anasikia atakutendea vyema hakika kwa majira na wakati unaofaa! 

Mungu akutie nguvu kusimama! 

Bwana akutendee vyema.

**by Melania Shedrack**

Leave a Reply