Hongera Jesca Wahuru: Mwenyekiti wa vijana mkoa wa Iringa (CCM)!

Jesca Wahuru: Mwenyekiti wa vijana mkoa wa Iringa

“Tareh 22.9 2017 Mungu aliweka historia nyingine kwenye maisha yangu. Ukijishusha Mungu atakuinua na ukijikweza Mungu atakushusha. Asanteni kwa kunikopesha kura zenu nawaahidi nitawalipa utendaji……..  Asanteni kwa kuniamini”~~~~~~~~~ Jesca Wahuru

Mimi siyo mwana siasa nawala sitegemei kuingia kwenye siasa maishani mwangu! Just show me where “money” is; I will meet you there! Better be 100% genuine though ?? I’ve my daughter and a life to live, for that prison ain’t my favorite place to be ??……….Ok! Back to our story! Japo mimi si mwana siasa lakini nina ndugu zangu ambao wanapenda siasa, na wengine siasa ndio carrier zao. Mfano mzuri ni huyu wifi yangu Jesca Wahuru, yeye ni Mwalimu kwa taaluma lakini siasa pia ipo kwenye damu yake. Anapenda siasa sana, na chama chake kipenzi ni CCM! Sasa juzi kati alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa vijana mkoa wa Iringa. Kwa maana hiyo naomba nichukue nafasi hii kumpongeza sana kwa hatua hiyo. Namuombea awe kiongozi mzuri ambaye ataweka maslahi ya nchi yake mbele na chama nyuma! UZALENDO! UZALENDO! Niwajibu wa kila raiya kuwa mzalendo kwa nchi yako, hivyo muwe wazalendo! Hongera sana. #WanawakeTunaweza

Leave a Reply