Happy birthday mama Salome!

Nyumba aliyokuwa anaishi mama Salome na watoto wake
"Maisha ya kila mwanadamu yana historia yake. Ndugu zangu ebu niwape history fupi wapi nimetoka ?. Hapo ndipo alipokua anaishi Mama yetu. This is our House?Jamani msinichukulie poa, sijakulia chips kuku mimi wala sausage ??. Vitu hivi nimekuja kuvijulia ukubwani; so when I say let me enjoy my life, let me enjoy bwana kwasababu I really deserve it. Niko proud na tulipotoka ? na tulipo sasa, mimi ni mtoto wa kwanza katika family ya watoto wanne and my Mom ni Nurse. Sasa why huyu Mama ananitoa machozi?? niko proud nae sana tena sana. Huyu Mama ni mwanamke muhimu sana katika maisha siachi kusema Mungu mpe maisha marefu Mama yangu maana pamoja na hali yake hii amehakikisha wote sisi tumeenda shule?alipambana na kila kitu ili sisi tukue.?? Dah! nashindwa hata kuandika ?....... Sasa basi Leo ni Birthday ya Mama yangu. Katika maisha yangu ya kawaida hii hali ya maisha yetu ilinisukuma sanaa tena sanaa mimi kufanya kazi kwa bidii maana nilijua mimi Ndio mkubwa nina wadogo zangu nyuma, kila siku nikawa napiga goti na kumwambia Mungu nisaidie nisikate tamaa katika biashara zangu. Nilitembeza nguo barabarani nilipita kila kona bila kuona aibu wala kujali nani ananicheka kumbe najua nini nafanya na nini nataka! Kuna vitu vingi nilitamani na nilikua na-dream navyo lakini kikubwa nilitamani na kumuomba Mungu amuweke mama yangu mpaka siku moja aje afurahi na kucheka katika maisha yake yote yaliyobaki mpaka anaingia kaburini ? Imagine mama Nurse wa kawaida sana akiwa na watoto wanne lakini alitulea, kama single mama katika kila namna tusikose maihitaji ya muhimu.......... maisha yetu yamenisukuma sana kufanya kazi kwa bidii ? Mama, Mama, u deserve something ?....Can't wait ?" ~~~~~~ Salome akielezea hisia zake

"Once again Happy Birthday mama yangu? as your first daughter sijui ni kitu gani cha kukupa ili uwe na furaha katika maisha yako yote na ukasahau machungu yote uliyopitia. Niliwaza sana nikupe nini mama yangu ?? Nikawa sipati jibu je nikupe Range Rover ??? nikagundua Hapana! Nikawaza je nikununulie V8?? Nikasema No Kwani ni Sh ngapi hiyo???????‍♀️??‍♀️ basi nikasema ebu nikupe heshima unayodeserve katika maisha yako yote. Today I decide to give you the Gift of the New House.?? Pumzika hapa Mama yangu enjoy maisha kipenzi chetu. Once Again Happy Birthday Mama Salome" ~~~~hayo ni maneno yake Salome

Mama yake Salome akimshukuru Mungu kwa mibaraka yake
Salome akilia kwa furaha huku mama yake mzazi (kushoto) pamoja na mama yake mkubwa (kulia) wakiwa sambamba naye
Mama Salome akiwa na watoto wake

Siwajui hawanijui lakini nimevutiwa na kuguswana story yao nikaona ni vyema ku share nanyi. ……….Happy birthday mama Salome. Nakutakia furaha zaidi, amani tele, na afya njema. Mzidi barikiwa. …….Hongera sana Salome!

Leave a Reply