Toni Braxton akubali pete ya Mr Birdman

Je, wewe unampenda mtu kwa muonekano wake, taiba, familia aliyotoka, akili zake, sura, pesa, jinsi anavyokuonyesha heshima n.k?  Mwanamuziki Brian a.k.a The Birdman  anasema "so what? What that gotta do with love?"  Hayo yalikuwa ni maneno yake baada ya Talk show host Wendy Williams kusema kuwa yeye alikuwa mtu wa kwanza kusema "hapana" aliposikia Toni Braxton ana mdeti The Birdman! Wendy amemueleza Mr Birdman kuwa muonekano wake na Toni ni tofauti sana hapo ndipo Mr "The Birdman" akasema vinahusiana nini na kupenda?! Yeye ni 'certified gangsta' ?? aliye kuzwa na street kwasababu mama yake alikufa akiwa na miaka miwili (2), baba naye japo hakuwa sana kwenye maisha yake naye alikufa, kaka, dada, bibi, babu wote wamekufa hivyo vitu hivyo vinemfanya asijue nini maana na thamani ya upendo lakini siyo kwamba hajui kupenda!  "I’m just a gangster, that don’t mean nothing. Certified too. What that gotta do with love?" Wendy alishikwa na kigugumizi baada ya jibu hilo! 

Hilo nalo ni somo kwa wengi wetu tunaopenda kusema "kampendea nini?" Wewe ukiona watu wanapendana kama huna jema lakusema nyamaza lakini ukitaka kujua kampendea nini utaumbuka kwani hayo ni ya Ngoswe muachie Ngoswe mwenye! Kila mtu ana kitu chake ambacho anatafuta katika kumpenda mtu sasa mambo ya kujifanya  mimi sijui "Engineer" ooh mimi "mfanya biashara" sijui msomi gosh!! What that gotta do with love?!! Kwani siku ukiwa huwezi kunyanyuka kitandani hizo degree zako zitakunyanyua kitandani? ?? Watu wanaangali potential ulizo nano! Unaweza ukawa mzuri na elimu nzuri lakini akili ya maisha hauna azidi ya kutaka kuwa "trophy wife" au "Mario" ulishwe na kuvishwa na mwanamke halafu bado utake uitwe mume ? anyway, Birdman amemvisha Toni pete yenye thamani ya $5,000,000

The Birdman siyo mwanaume pekee ambaye anatarajia kufunga ndoa na mtu ambaye watu wengi walidhani haiwezekani.  Prince Harry naye mwaka jana mwishoni alimvisha pete ya uchumba muigizaji wa kimarekani ajulikanaye kama Megan Markle. Kwa hapa Megan ni mkubwa kwa Prince Harry kwa miaka mitatu (3yrs) na pia huko nyuma alishawahi kuolewa na kuachika. Ndoa yake ya kwanza ilidumu kwa miaka miwili (2 yrs) baada ya kudate kwa kwa muda wa miaka 6 ?? Hivi ndivyo vitu ambavyo sivielewi watu wadate kwa miaka sita halafu ndoa idumu kwa miaka 2 tu!! Tena hapo mpaka divorce imetoka ina maana atakuwa walitengana at least miezi 6 kabla ?‍♂️?‍♂️ Haya huyu Prince Harry ame mvika pete baada ya kumdate kwa muda wa miezi 15 (sawa na mwaka mmoja na miezi 3). Je, nitakuwa sahihi kusema ngoja tuone hii itadumu kwa muda gani au tuwatakie kheri tu ?

Btw, hata Toni Braxton hii itakuwa ndoa yake ya pili! Ndoa yake ya kwanza ilikuwa na mwanaume mwenye asili ya ngozi "nyeupe" ilidumu kwa muda wa zaidi ya miaka kumi na mbili (12  yrs) na alizaa watoto 2, Toni ana miaka 50 sasa.....Haya wale tunao pendeza hii show ya Braxton Family Values ndio tutakao faidi uhondo wote ? Siamini siku hizi nimemuambukiza mama yangu kupenda hizi show ?? anajua mpaka ratiba zake ??

Leave a Reply