Mwanamke wa Shoka 2018: Jiamini, Jitambue, Jikubali, Chapa kazi, Songa mbele

Regrann from @dinamarious - Sio kila jambo ni baya....wakati mwingine jambo zuri huanza kama baya....lakini baadae linakuja kukaa sawa katika uzuri wake unaostahili. Mwanzo wako unaweza kuwa mbaya lakini ikaja kuwa uhondoooooo. Changamoto zako zinaweza kuwa ngumu lakini kumbe baraka zako na mafanikio yako ndani ya changamoto hizo.

Inapofika mwezi wa tatu shamrashamra za kuelekea siku ya wanawake duniani huanza.Kubwa ni kusherehekea mafanikio,kutiana moyo na kupigania haki ya mwanamke hasa wale wanaonyanyasika.

Wanawake tunapitia changamoto nyingi sana lakini napenda nikwambie jifunge mkanda...pambana hakuna kujihurumia...dada utafika twende tukutane kwenye kilele.

Mwanamke wa Shoka.....jiamini, jitambue, jikubali, chapa kazi, Songa mbele tukutane Kileleni tuchape kazi ???
#Mwanamkewashoka2018 - #regrann

Leave a Reply