Hot shot of the day

FB_IMG_1440181860328Mr President!  Safi sanaaaaaa, sio kama wakina “fulani” wakienda likizo wanaishi Dar hawakumbuki hata bibi na babu zao kijijini eti kisa wanakaa sijui U.S.A au Ulaya kha! Kuishi nje ya Tanzania sio sababu ya kutokuthamini wakwenu hata kama ni masikini kiasi gani!

Wengine mpaka wanatafuta mama / baba na ndugu wa bandia, wanajiona hawawezi kuwa na undugu na wakwao kisa wanaishi majuu!! Mmmh! Halafu sasa wakitokea kwenda kusalimia huko vijijini  au “uswahili” (kama waitavyo) wanakaa kwa masaa machache hawasaidii kazi yoyote ile; hata kuosha vyombo hawasaidi ?? jamani tujifunze kutoka  kwa watu kama Mr. President! Ubarikiwe sana.

Kwa faida ya wasomaji huyu ni Iddi Sandaly maarufu kama Mr President. Ni President wa jumuiya ya Watanzania wa DMV.

Leave a Reply