Housegirl kaalikwa ubalozi wa Marekani!

Tukiwa bado tunasherekea mwezi wa Superwomen duniani, basi siku ya juzi nikakutana na post ya Superwoman Joyce Kiria kama isomavyo ????

Reposted from @joycekiriasuperwoman Basi leo nilipata Fursa ya kualikwa na Ubalozi wa Marekeni kwenda kushea Safari yangu ya maisha katika kuendeleza Sherehe za Siku ya Wanawake Duniani 2020..Nilikuwa na Masupa Wuman wenzangu hawa hapa, Mercy Kitomari mwenye IceCream zake mjini, MD wa Lake Fm Noreen, Neema Md wa Penuel Investment, ..Aisee Nimegundua safari yangu ya maisha inasisimua na inahamasisha sana kupambana bila kuchoma, safari yangu ni nguvu ya Mwanamke hasa binti ambae anaanza kutafuta maisha…. nitaisimulia tena na tena coz I am a Super Woman ???? Stay tuned ??? Nitagie hawa masupa woman ???..Asante sana Ubalozi wa Marekani ??? – #regrann

Joyce Kiria akiwa na Superwomen wenzake walio alikwa ubalozi wa Marekani, Tanzania

Kwanza kabisa nianze kwa kusema hongera sana Joyce Kiria kwa mualiko huu! Kama nilivyo sema kwenye kurasa yako kuwa “what a milestone”! Unastahili!

Pili, naomba Watanzania mjifunze kutoka kwa wenzenu ambao wametoka katika nchi zilizo endelea. Mnaona jinsi gani wanavyo heshimu wapambanaji wa aina zote bila kujali elimu zao! Sidhani kama hizi nchi zingeendela kwa kubagua mtu au kitu chochote kile ambacho kina uhai, ndio maana huku kuna mifumo ya kusaidia na kuelimisha hata watu wenye utindio wa ubongo (matahaira), huku kuna haki za wanyama hadi Paka! Ndio maana wazungu waligundua Kia iki wapige hatua na kuendelea kuwa na nguvu ya kutawala dunia lazima ubaguzi na biashara za watumwa zikome! Maana walijua hatoweza kuendelea kwa kubagua fungu la watu fulani ambao wako ndani ya ardhi yao!

Mara nyingi unakuta baadhi ya Watanzania wanapenda kuona mtu ambaye ana “Masters” au “PhD” au anayejua kuongea Kingereza ndio mwenye akili ya kufanya vitu vizuri na vikubwa ambavyo watamuangalia kama “Role model”! Yani wanaona mtu aliye fanikiwa kwakupitia “structured” system basi huyo ndio anatakiwa kuwa role model na inspiration person wao! Watu kama akina Joyce Kiria ambao wamepata elimu na kupambania ndoto zao katika mifumo isiyokua rasmi wao wanakua hawana maana mbele ya hawa watu wanaojiita “wasomi”! Hata serikali yetu haiwatambu na kuwapa uzito watu wenye history ya maisha kama ya Joyce Kiria. Yani ni mentality fulani ya kuhuzunisha sana. Embu ona Kim Kardashian West anavyothaminiwa hapa Marekani, anauwezo wa kuweka appointment na kuonana na Rais kuongea juu ya maswala muhimu yanayohusu nchi yao. Everyone has something to offer, we need to learn to respect one another!

Wakiambiwa leo hii watoke hadharani watu wangapi ambao wanajiita “wasomi” nawamuangalia Joyce Kiria kama “Role model” wao?! Sidhani kama kuna hata mmoja atajitokeza! Siyo kwamba hawamjui au hawatizami kipindi chake hapana! Nikwasababu tu nakwenda shule kwenye mpangilio uliopangwa na serikali (jamii), mafanikio yake hayakutokana na ‘elimu’ hivyo wanamuona kwamba ni mtu fulani asiye na thamani ya (she is beneath) kua miongoni mwao! Hapo ndipo utasikia aah! Mie namuda wa kumuangalia housegirl? ?? nahivi sio member wa Chadema basi ndio tobaaa ?? Wakati ukweli ndani ya mioyo yao wanatamani wangekua na courage kama ya Joyce! Kwanza kumbuka huyu sasa watu wanasema “ALIKUWA Housegirl” keynote hapao ni ALIKUWA, she no longer exist in that title! hiyo ni history tu sasa! It defines where she came from but not her destiny! Haya housegirl huyo ndani ya American Embassy tena kwa mualiko maalum! #Respect people’s hustles! Kama ingekua Mungu anaangalia history ya mambo ya watu basi tusingekua na BiBle! Maana vitabu vingi ndani ya Bible vimeandikwa na watu ambao walikua wadhambi kweli kweli!

Joyce Kiria

Mimi Joyce ni mmoja ya watu wanao ni inspire, kwakweli ni mwanamke shujaa! Japo siwezi muita “role model” wangu, kwani binafsi huwa nasema na huu ni mtazamo wangu mimi Alpha; Katika dunia hii sina mtu yoyote yule ninaye muita “role model” wangu zaidi ya Yesu Kristo! Nina watu wengi wana ni inspire katika mambo mbali mbali na wakwanza kabisa ni wazazi wangu! I never call anybody in this planet my “role model”, kwani huyo ni mtu unayetamani kua kama yeye, nami kama kuna mtu natamani nifanane kama yeye basi si mwingine bali Yesu mwana wa Mungu! I want to be like Jesus!

Nilichogundua Watanzania wengi wenye elimu haswa hawa wakizazi hichi cha kwetu wapo very ignorance na wanachuki sana na watu ambao wamefanikiwa bila kupitia mfumo rasmi ya elimu (structured education). Haswa hawa watoto walikua, kusoma, na kutanua maisha kwa kutumia kodi za wananchi! Utakuta wazazi au mzazi wao alikua Mbunge / waziri / au senior Government officer basi wakiona mtu kama Joyce ambaye baba yake hukuwahi kua hata katibu kata amefanikiwa basi roho zinawauma wanakua na chuki kibao ?? Sikiliza wewe msomi, wewe unakipaji kwasababu kuna mtu katumia muda wake kukujaza madini kichwani mwako! Ingekua hauna hiyo elimu uliyopata darasani huwenda ungekua ni Zero brain! Mtu kama Joyce amejaliwa kipaji na uwezo mdogo wa elimu ambacho kimemfikisha hapo alipo ambapo wewe mwenye elimu umeshindwa kufika! Embu fikiria kama Joyce akiamua kuongeza elimu kidogo tu, itakuaje?! Unafikiri kuna msomi yoyote atakaye mbabaisha! Respect people’s hustles siyo elimu! Hata Bill Gates hakumaliza shule itakuwa Housegirl! Elimu ya darasani ni nzuri sana na ni muhimu lakini elimu ya ubinadamu (UTU) ni muhimu zaidi!

Marehemu Ruge Mutahaba akielezea kwa uchungu jinsi wasomi wa Tanzania walivyo small-minded, they think so shallow! Na hili tatizo huwa linanishangaza sana! Anyway, R I. P Legend, tutakukumbuka daima!

Kila tatizo lina chanzo chake kama ilivyo kwa jambo jema. Viongozi ambao mnatizamwa kama kioo cha jamii mnatakiwa muanze kuonyesha mfano wa UTU wa kuthamini kila mtu bila kubagua uwezo wake wa kuelimisha! Huku kwa walio endelea, utakuta viongozi wa juu hata Rais anatembelea shule yenye watoto wenye utindio wa ubongo, ili akiwa anafanya maamuzi au kuongea awe anaongea kitu anacho kijua na sio kusimuliwa na mtu, ambapo utakuta hata huyo mtu aliyekwambia naye kasimuliwa tu! Senator anaopopeleka mswada wa kuomba kuongeza pesa za kuelimisha watoto ambao ni Autist, anakua teyari anaelimu tosha juu ya Autism na umewaona kwa macho yake kua Autist anaweza kufundishwa kwa level ya uwelewa waka na akafundishika kabisa na kuwa independent! #Tubadilike

Kwa mara nyingine tena hongera sana Joyce, safari ndio kwanza umeanza, nakutakia mema yote!

Leave a Reply