Je ulishawahi kufanya makosa kama yangu?

 Watu wengi wanatabia ya kupenda kuhisi vitu au kumuhisia mtu badala ya kumuuliza muhusika ili wajue ukweli! Hiyo caption kwenye picha ya Dina Marios imenifanya nikumbuke makosa yangu niliyowahi kufanya huko nyuma. Dina ameweka caption ?? isemayo "Msomali wa Kihaya"  kitu ambacho kimenishangaza kidogo kwani siku zote mimi nilihisi kuwa Dina ni Mchaga ?? Sijui kwanini lakini hivyo ndivyo nilivyo muhisi!   

@Regranned from @dinamarious – Msomali wa kihaya
#VipichaPicha
 Sasa haya mambo ya kuhisi vitu kwakweli siyo mazuri hata kidogo kama unayo hiyo tabia basi kuanzia leo anza kujifinza kuuliza kwa kila jambo ambalo hujui kwani itakusaidia sana! Mimi nilipokuwa secondary mmoja wa rafiki zangu alikuwa anaitwa Msolwa Mgawe, sasa huyu Msolwa kwa muda wote tupo shule sikuwahi kumsikia akimtaja baba yake katika maongezi yake. Utasikia kamtaja mama, kaka, na dada zake lakini si baba yake hivyo kwa akili yangu yakupenda kuhisi nikahisi kuwa huwenda baba yake alikwisha fariki hivyo hataki kumuongelea ?? ............ Sasa siku mmoja katika story sijui tulikuwa tunapanga kufanya nini ila akasema kuwa  yeye hatoweza kwani "mshua leo anarudi" akimaanisha baba yake anarudi! Nikashangaa, ikabidi nimwambie kuwa mimi nilihisi baba yake amefariki miaka mingi kwani sijawahi msikia akimuongelea baba yake! Yani group zima lilikufa kwa kicheko ??? Msolwa akasema Alpha sidhani kama una akili timamu ??? ..............Jamani kuuliza si ujinga bali ni kutaka kujua, na hata siku moja hakuna swali la kijinga isipokuwa wajinga ndio huwa hawaulizi maswali! Hacha kuhisi vitu au kumuhisia mtu kitu siku zote kama unaweza uliza but don't assume!! Kuhisi ni kubaya sana!

Leave a Reply