Kesha la asubuhi: Hata watoto wanaweza kushuhudia imani yao

                  *KESHA LA ASUBUHI*

                           JUMATANO

                           13/06/2018

          _HATA WATOTO WANAWEZA

            KUSHUHUDIA *IMANI* YAO._? *“Lakini wakuu wa makuhani na waandishi walipoyaona maajabu aliyoyafanya, na watoto waliopaza sauti zao hekaluni, wakisema, Hosana, Mwana wa Daudi! Walikasirika, wakamwambia, Wasikia hawa wasemavyo? Yesu akawaambia, Naam; hamkupata kusoma, Kwa vinywa vya watoto wachanga na wanyonyao umekamilisha sifa?” (Mathayo 21:15, 16).*

✍?Bendera ya neno la kweli inaweza kuinuliwa na wanaume na wanawake wanyenyekevu; na vijana, na hata watoto, wanaweza kuwa baraka kwa wengine, kwa kudhihirisha kile ambacho kweli hiyo imewafanyia.

✍? Mungu atawatumia mawakala dhaifu zaidi ikiwa wamejisalimisha kikamilifu Kwake. Anaweza kutenda kazi kupitia wao ili kuzifikia roho ambazo mchungaji asingeweza kuzifikia. Kuna njia kuu na vichochoro vinavyopaswa kuchunguzwa. Mkiwa na Biblia yenu mkononi mwenu, moyo wenu ukichangamka na kung’aa kwa upendo wa Mungu, mnaweza kuondoka kwenda kuwaambia wengine uzoefu wenu;

✍? mnaweza kuwajulisha kweli ambayo imeugusa moyo wenu, mkiomba kwa imani kwamba afanye jitihada zenu ziwe na mafanikio katika wokovu wao. Wasilisha nuru, nanyi mtapata nuru zaidi ili kuwasilisha. Kwa namna hiyo mnaweza kuwa watendakazi pamoja na Mungu.

✍?Mungu anatamani kwamba watoto Wake watumie juhudi zao zote, kwamba katika kutenda kazi ili kuwabariki wengine, waweze kuimarika katika nguvu ya Yesu. Mnaweza msiwe na elimu; mnaweza msifikiriwe kuwa na uwezo wa kumfanyia Mungu kazi kubwa; lakini yapo mambo mnayoweza kufanya. Mnaweza kuifanya nuru yenu iwaangazie wengine.

??‍♂```Kila mmoja anaweza kupata ufahamu wa neno la kweli, na kuwa na mvuto mwema. Hivyo nendeni mkafanye kazi, ndugu na dada zangu. Jipatieni uzoefu kwa kufanya kazi kwa ajili ya wengine. 

??‍♂Mnaweza kufanya makosa; lakini hili haliwezi kuzidi kile ambacho wale wenye maarifa zaidi, na wale walioko katika nyadhaifa za mamlaka, wamefanya tena na tena. Hamtapata mafanikio wakati wote; lakini hamwezi kamwe kujua matokeo ya juhudi duni, isiyotafuta manufaa binafsi ili kuwasaidia wale waliomo gizani. 

??‍♂Kupitia utendaji wa Roho Mtakatifu, mnaweza kuongoa roho kutoka gizani kuja kwenye kweli, na kwa kufanya hivyo roho zenu wenyewe zitajawa upendo wa Mungu.```

*MUNGU AWE NANYI MNAPOTAFAKARI*

Leave a Reply