Kesha la asubuhi: KUTAFUTA HAZINA

KESHA LA ASUBUHI 

    IJUMA  6/4/2018

                   _KUTAFUTA HAZINA_ ✍*Tena ufalme wa mbinguni umefanana na hazina iliyositirika katika shamba; ambayo mtu alipoiona, aliificha; na kwa furaha yake akaenda akauza alivyo navyo vyote, akalinunua shamba lile. Mathayo 13:44.*Kwa kiasi kikubwa, katika siku zetu hizi, kanisa limekuwa likiridhishwa na ukweli wa ufunuo unaoonekana juu juu, ambao umefanywa kuwa wazi na rahisi kueleweka kiasi ambacho wengi wamedhani huu umeshaeleza yote yaliyokuwa muhimu, na katika kuukubali wameridhika. Lakini Roho Mtakatifu, anapotenda kazi moyoni, hatauruhusu utulie katika uvivu.

✍Huwa anaamsha shauku ya dhati kwa ajili ya ukweli usiochafuliwa kwa makosa na mafundisho ya uongo. Ukweli wa mbinguni utamtuza mtafutaji wa kweli. Moyo ambao una shauku ya kweli ya kujua kweli ni nini, hauwezi kuridhika katika uvivu.

✍?Ufalme wa mbinguni umefananishwa na hazina iliyofichwa shambani, “ambayo mtu alipoiona, aliificha; na kwa furaha yake akaenda akauza alivyo navyo vyote, akalinunua shamba lile.” Anainunua ili apate kuifanyia kazi, analima kila sehemu yake na kuchukua vile vilivyo katika hazina yake. Kuongoza utafiti huu na kuutuza ni huduma ifanywayo na Roho Mtakatifu. 

✍?Mtafiti, anapokuwa akililima shamba anakutana na mkondo wa madini ya thamani ambayo anajaribu kukadiria thamani yake, naye hudidimiza mtarimbo chini zaidi, kwa ajili ya hazina zaidi yenye thamani. Kwa namna hiyo tabaka kubwa zaidi la madini hugunduliwa. Maeneo ya dhahabu ardhini hayakusokotana na mikanda ya mawe ya thamani kama lilivyo shamba la ufunuo lenye mikanda inayodhihirisha utajiri wa Kristo usiochunguzika.

??‍♂ ```Ni shauku ya Bwana kwamba kila mmoja wa watoto wake wanaoamini awe tajiri katika imani; nalo hili ni tunda la utendaji wa Roho Mtakatifu moyoni. Kutokea moyoni, Roho hutenda kazi akielekea nje, akiendeleza tabia ambayo Mungu ataikubali.```

??‍♂ ``` Shamba la hazina za ile kweli ambazo Kristo aliongeza kwenye milki ya imani ili wanafunzi wapate kujitwalia ni kubwa kiasi cha ajabu! Tunahitaji imani kubwa zaidi kama tunahitaji kuwa na ufahamu bora wa Neno. Kizuizi kikubwa zaidi katika upokeaji wetu wa nuru ya mbinguni ni kwamba hatutegemei ufanisi wa Roho Mtakatifu. – Ellen G. White 1888 Materials, uk. 1537, 1538.```

*MUNGU AWABARIKI MUWE NA SIKU NJEMA.*KESHA LA ASUBUHI 




Leave a Reply