Madafu!

194x140xcoconut-palm-1.jpg.pagespeed.ic.QEjUwX8bHHJe unajua faida za kunywa maji ya Madafu? Ngoja kwanza nianze kwa kushudia mimi mwenye kuwa nashukuru roho aliyeniongoza nikaanza kutumia maji ya Madafu! Ilinitokea tuu nikiwa kwenye International market grocery store nilikuwa nina njaa sana na pia nilikuwa na kiu. Sasa sijui kama wewe imeshawahi kukutokea pale unapokuwa na njaa sana yani hata maji unaona machungu kabla hata ya kunywa ?

Sasa hapo ndiyo nikaamua kununua maji ya Madafu (Coconut water) ambayo ni 100% pure Madafu, ni kapenda sana. Basi nikanunua box 3 nikuwa na mpango wa kunywa kama juice. Nilipofika kwenye ‘kibanda’ changu nikasoma yale maandishi yanayo andikwa kwa pembeni mwa box. Nikaona wamesema you can use it as sweetener kwenye Chai au smooth badala ya kutumia Sukari. Basi nikaamua kujaribu kuweka kwenye chai, jamani wapendwa mimi hadi leo ni 3 weeks sijagusa Sukari kabsaaa! Yani naweka maji ya Madafu kwenye kikombe nachanganya na maji yamoto naweka na jani langu la green tea  mchezo umeisha! 8-Benefits-of-Coconut-Water-You-Didnt-Know-About-380x213

Mimi nilikuwa nimekatazwa na ma-doctors nisit mie kabisa Mchele (rice) na Sukari kwa muda sasa. Lakini Mchele nilifanikiwa kuacha yani kama nikila ni huwa nipo nje ya ‘kakibanda’ changu ☺ ila mimi mwenye hata huwa sifikiri kupika! Sasa kasheshe ilikuwa kwenye Sukari ? Yani ilikuwa ngumu sana haswa kwa sababu kuu mbili: kwanza mimi ni mtu ambaye napenda kunywa chai sana na Asali sipendi taste na harufu yake hivyo sukari ndio ilikuwa natumia. Pili na ishi Michigan  ?  state ambayo inakuwa na baridi kali na kwa muda mrefu hivyo watu wengi huwa wana kuwa na some sort of depression kwahiyo Sukari is the best comfort food naipo easily accessible. Hivyo nilijikuta nashindwa kuacha Sukari kabisa mpaka nilipo pata Madafu.  Yani sasa hivi nikijisikia nipo down basi nakunywa maji ya Madafu na kwakweli  it refreshes me alot!

Wataalam wanasema kunafaida nyingi za kunywa maji ya Madafu na hizi ni baadhi tuu

1. Ina colories chache sana, cholesterol free, na ina potassium nyingi sana zaidi ya kula ndizi nne kwa mara moja. Hivyo kwasababu ya hizo nutrients ambazo inazo inakuwa inauwezo wa kukusaidia katika maswala ya kupungua uzito wa mwili. Na huwa humfanya mtu ajisikie ameshiba kwa muda mrefu.

2. Inasaidia kuondoa chunusi kwenye ngozi ya uso. Hapa ukiwa kila siku hasubuhi kabla ya kula kitu chochote halafu inabidi upunguze vyakula vyenye mafuta.

3. Inasaidia kupungua / kutibu Bp (Blood pressure)

4. Ina up a mwili nguvu na kusaidia upungifu wa maji mwili ni

5. Hii ni kwa wale wanao kunywa Pombe ? inasaidia hangover 2015-07-26 10.39.13

Haya wapenda kama utapenda kujaribu na kusihi anza na wala huto juta.

 

 

Leave a Reply