Mama na baba wa 8020Fashion blog katika ubora wao! #ZezeTV

Sasa sikiliza, niliona hii short video kwenye Instagram  ya Shamimu Mwasha kuhusu kwanini wanawake  hatuna ujasiri wa kutongoza wanaume? Yani hata kama umemuona mwanaume unaye mpenda huwezi kumtokea na kumwambia?? embu msikilize ??
Basi nikaona kuwa video ni fupi nikasema ngoja niende YouTube nitafute labda nitapata yenye full length! Too bad sijapata lakini nikakutana na hii video nyingine ambayo mama wa Zeze TV akitengenezwa nywele na mumewe Abdul Nsembo! Embu itizame kwanza ??

Jamani si wamependeza eeh! Halafu eti Shamimu kamuitaje mumewe?? Mie nimejaribu kurudia mara kadhaa lakini sijamuelewa ??.........Nani alikwambia wakaka wa Kibongo hawajui kupenda?! Wapo wanaojua kupenda kwa dhati kabisa simnamuona Dr. Mengi na Jackie wake, na sasa Zeze na Abdul, haya subirini na mimi na Muhaya wangu mtakoma wenyewe ?? Sasa hivi bado tunajifunza mapozi ya picha na kuongea simnajua lazima nitoe hii accent ya Kijaluo ???
Anyway, nice video mama ZezeTV. Ninejifunza kitu fulani juu ya nywele fupi za twist, kazi yake yataka moyo kwakweli! Maana vitu vilivyopakwa humo si mchezo! Lakini naipenda sana, Shamimu huwa anapendeza sana na hizo nywele......halafu you got really beautiful voice! ❤

 

Leave a Reply