Mjane wa Deo Filikunjombe awashukuru Watanzania!

Screenshot_2015-10-29-19-57-27-1Kwakupitia account yake ya IG mjane wa Filikunjombe ametoa shukran zake za dhati kwa Watanzania wote walioguswa (kuna wengine hawakuguswa kama Joyce Kiria) na msiba wa mumewe. Amesema yeye hana chakuwalipa kwa upendo na ukarimu walio muonyesha. Pia wale ambao hawakuguswa na kifo cha mumewe nao amewashukuru. Na wale ambao hawakuguswa nawakaona njia pekee ya kumfariji ni kumuongezea machungu kwa kumuongelea mme wake vibaya nao amewashukuru kwa kusema amemuachia Mungu! Soma ujumbe wake hapa chini ?      Screenshot_2015-10-29-17-41-44-1 Mjane wa Filikunjombe ameumizwa sana na maneno ambayo Joyce Kiria wa Wanawake Live Show aliyasema kwenye social media kuhusu nyumba ya marehemu. Joyce bila huruma wakati watu wakiwa wanakusanyika kwa msiba wa Deo pale nyumbani kwake Mtomi Kijichi aliandika post ambayo ilikuwa ikionyesha nyumba ya marehemu na nyumba mbovu ya manyasi kama mfano wa maisha ya mwanasiasa wa CCM na maisha ya Mtanzania wa kawaida! Hiyo post aliandika kama ifuatavyo:- ? Screenshot_2015-10-26-19-29-34Joyce Kiria, wewe unajiita “Super Woman” kwakweli mimi nakuita ‘Super Mchawi!!’ kwani uliyo yatenda ni uchawi mtupu!! Yani wewe mwenzako kafiwa na mumewe katika ajali mbaya namna ile, kaachwa mjane wakati angali “mdada mbichi” kabisa na watoto wadogo watatu wote wakiwa chini ya miaka kumi na nane!! Lakini hayo yote hukuona cha kuongelea isipokuwa nyumba yao?! Kweli?? Unajua mchawi si lazima atembee na hirizi na tunguli shingoni bali matendo na maneno yake yanatosha kuwa mchawi!! Na wewe ume-qualify kuitwa Mchawi!! Jifunze kufurahia maendeleo ya wengine, bariki wengine nawe utabarikiwa. Kila mtu anafungu lake ambalo Mungu amemuandalia; lini na wapi atakupa hiyo ni siri yake Muumba! Kwahiyo usiumie sana kuona wenzako wamebarikiwa sasa kama nawewe ungeacha roho ya kichawi labda Mungu naye angekubariki wakati huu. Lakini kwa roho hii utangoja sanaaa!! Halafu hujui watu wamepitia wapi mpaka kufika hapo walipo ‘when you see the glory ask for their story!’ Shame on you!!

Pole sana mjane na watoto wako, pamoja na ndugu, jamaa, marafiki, na Watanzania wote. Mungu awape faraja na nguvu ya kuhimili kipindi hiki kigumu. R.I.P Mh. Deo Filikunjombe.

2 thoughts on “Mjane wa Deo Filikunjombe awashukuru Watanzania!”

  1. Poleni sana Mpendwa naomba ukae kwa Amani na subra,yote hayo ni mitihani pia hua ni mapito Daima muweke Mungu wako mbele ktk kila jambo lako hakuna mshindi wa haya Maisha,ukweli unajua wewe peke sio mtu mwingine yoyote Yule,kaa kwa Amina ‘Mpendwa (ktk Maisha kukaa kimya bila kujibu ni jibu tosha sana usimpe kiumbe nafasi ya kujibu)bye!!

Leave a Reply