Mjukuu namba moja atua Dar!

Mjukuu namba moja akiwa na mama yake

Tarehe 28 ya mwezi wa Saba, mwaka huu wa 2021 mjukuu namba moja alipanda ndege na kuanza safari ya kwenda Tanzania ?? kusalimia bibi, babu, wajomba, mashangazi, mama wadogo kwa wakubwa,

Sambamba na mama yake mjukuu namba moja akiwa katika maeneo ya kiwanja cha ndege cha George Bush Intercontinental Airport kabla ya kupita kwenye bench la watu wa usalama na kuelekea kwenye terminal waliokua wakiondokea.

kwa kupitia ukurasa wake wa Instagram na Facebook mama yake mjukuu namba moja aliandika maneno haya “Safari njema Mungu awe nawe! Salimia bibi, babu, mashangazi, wajomba, ndugu, jamaa, na marafiki! ♥” ambayo yalikuwa yakimtakia safari njema binti yake!

Mungu ni mwema sana, kwani mjukuu namba moja amefika salama Dar es salaam, Tanzania majira ya saa tano usiku (11.00pm) kwa ndege ya KLM iliyopita Amsterdam, Zanzibar, na kisha kutua Dar.

Blessing akisubiria kumpokea best ake

Ndugu wakiwa na furaha ya kumuona mpendwa wao baada ya miaka 2 yakutoonana uso kwa uso. Mungu azidi kupewa sifa. ??

Mtu na mtu wake! Mashosti! …. Bibi na mjukuu namba moja!

“Ni asubuhi njema na yenye furaha, Uzao wa Uzao wetu, atua Plot No. 10.. &1..0, Utegi Street – Kibada saa saba usiku. Tumshukuru Mungu kwa kumfikisha salama kutoka Houston,Texas.” **** Sir O.O Igogo Maneno ya babu yake mjukuu namba moja.

Haya basi, namtakia mapumziko mema. Ngoja adeke kidogo kwa bibi na babu. Nakumbuka enzi babu yangu na bibi zangu wakiwa hai, siku zote nikifika Tanzania ?? lazima niende kijiji kuwaona na kudeka kwingi. Ni mwendo wa kuchinjiwa Mbuzi na Kondoo tu! ?? Nawakumbuka sana, waendelee kupumzika kwa amani. ??

Leave a Reply