Muhtasari -sehemu ya 3: Familia yakutana.

Baba na binti zake

July 31st, 2022 siku kadhaa baada ya mimi kufika nyumbani wanafamilia walikusanyika kwaajili ya kusalimiana na kufurahia pamoja kama familia. Zifuatazo ni baadhi ya picha na video ya siku hiyo.

Baba na wanawe

Yani hapo juu ni picha hadimu sanaaaaaaa! Kitendo cha kaka yetu mkubwa kuwepo kwenye picha ni kitendo kinachotekea kwa NADRA mno. Hapendi kupiga picha kabisa yani hata hapo tulimlazimisha kweli akaona aibu akakubali 😅😅

Mzee 0.O Igogo na kaya zake 😍
Mabinti wa marehemu mzee Cornel Awiti

Pichani juu ni mama yangu mzazi na wadogo zake wa tumbo moja. Warembo wa marehemu mzee Cornel Awiti na marehemu Valeria Awiti, hapo wamekosekana mabinti watatu tu nao ni; Felista Awiti (Mrs Joseph Musira) huyu ndio wakwanza kuzaliwa. Wapili kuzaliwa ni Mwalimu Anna Awiti (Mrs. John Obure), na Yacinta Awiti (Mrs Amos Onditi) huyu kuzaliwa ni wapili kutoka mwisho kati ya watoto 18. Mtoto wa mwisho kuzaliwa ni huyo mwenye gauni lenye maua meusi na meupe hapo juu anitwa Julia Awiti (Mrs Airo).

Wakwe nao hawakubaki nyuma 😍😍 Mmoja hakuwepo ila aliwakilishwa vyema na mkewe (dada mkubwa) mwenye gauni la blue.

wajukuu na babu yao
wadada katika ubora wetu

Twamshukuru Mungu kwa yote. 🙏🏿❤️🙏🏿

Leave a Reply