Mzee Igogo amkumbuka rafiki yake waudogoni!

"Rarafiki wa tangia udogoni, JAO NYAKWARAKONG'O - CPA Veteran, former Chief Accountant of NMC Ltd, NAPOCO Ltd, LIDA and then a free lancer External Accounts Auditor. Nilimkumbuka saana nikaamua kumtafuta asubuhi hii ya leo saa tatu nikatua getini kwake. Picha imepigwa na Mke wake Nyategi."~~~~ Sir O.O Igogo 

Je, unawakumbuka rafiki zako wa utotoni? Au maisha yako yakipanda kidogo tu na hata wale mlio kuwa wote habari nao huna tena? Sisemi kila rafiki au mtu uliyekuwa naye au kuishi wote mtaa mmoja lazima awe rafiki yako wamilele, hapana! Marafiki wengine hata kama mmetoka mtaa mmoja inabidi tu uachane nao haswa kama hawaleti amani na furaha maishani mwako. Hata mimi kuna watu tumekuwa wote mtaa mmoja au tumesoma wote shule lakini sasa hivi tukikutana tunasalimiana tu na kila mtu anaendela na maisha yake. Hamna shida kabisa! Lakini kuna marafiki ambao kwakweli haiwezekani kuwaacha hata kidogo au kuwasahau kabisa!! Tukumbuke marafiki zetu......pichani ☝ ni shemeji yangu na rafiki wa baba yangu ambaye walikuwa wote. Na jana alikwenda kumtembelea nyumbani kwake Tabata kama maelezo yake yanavyosema. 

Leave a Reply