Ndugu ni ndugu tuu!

Hakuna kitu kibaya kama kujidanganya nwenyewe; mimi naamini kuwa ni dhambi kubwa sana mwanadamu anaweza kujitendea hapa duniani “lying to yourself.” Kutokana na sababu mbalimbali watu wengi wanapenda kuonekana wamo kwenye group fulani, may be ni kwasababu ya life-style, income status, social status, e.c.t. Na mara nyingi watu hupoteza karama zao, au Mungu anashindwa kuwabariki kwa kwadri alivyotaka kuwabariki kwasababu tuu wameng’ang’ania sehemu fulani bila kujua kuwa hapo walipo sio mahala pao, au huwenda wange toka na kua true to themselves wangebarikiwa zaidi.

Shy-Rose-0
     Shy-Rose akiwa kijijini Majita. Nyumbani kwa wajomba zake alipo zaliwa mama yake mzazi.

Unaweza kujiuliza kwanini nimetumia picha ya Mh. Shy-Rose Bhanji, sababu ni kwamba kwanza namkubali (I just love her personality and character), pili narudi pale pale kwenye swala la kujidanganya. Ushawahi kuona watu ambao wanajidanga mpaka kuanza kutenga ndugu zao sababu tu yakuwa wana hali duni au wana elimu ya chini? Eti kwasababu sasa hivi anaishi mjini au nje ya inchi basi anatafuta ndugu wapya ambao anaona anafanana nao kimaisha na kabisa anaamua kujitenga na kukana ndugu zake. Kumbe bila kujua kutenda kwakwe hivyo kunamsababishia akose mibaraka mingi sana. Unaweza ukaona maisha yanakunyookea kwasasa lakini ukashangaa ghafla umerudi square zero halafu unabaki unajiuliza ni wapi umekosea. Au unakuta unapata ugonjwa wa ghafla ambao unahitaji huduma ya ndungu zako 24/7.

Basi tuige mfano wa dada yetu hapa Shy-Rose! Yeye hajaogopa kuwa tofauti na wadada wengi waishio mijini. Pamoja na cheo na umaharufu alio kuwanao bado anapenda na kuwathamini wa kwao bila kujali hali zao kiuchumi.  Tena zingatia kuwa hawa ni ndugu wa ujombani, na mama yake mzazi halisha lala usinginzi wa mauti, hivyo ilikuwa rahisi sana kwakwe kugeuza shingo yake na kuto kuwakumbuka tena ndugu wa marehemu mama yake. Na kikubwa sana ambacho nimeguswa nacho, ni kwamba hakuona aibu ku share na marafiki zake kwenye social media, ambapo wengine wangejifanya wao kwao wote ni matajiri hakuna watu wenye hali duni!

Shy-Rose-2
                                        Shy-Rose akisaidia kuandaa chakula na ndugu zake

Mnamo tarehe ya January 12, 2015 kuna rafiki yangu aliweka hii status kwenye facebook wall yake………………”Dawa ya kumkomesha mtu mwenye Majidai na Dharau kwa watu wahali ya chini ni Kumpa Dose ya Dharau Twice. Huwa nawapenda Sana this type of pple Wanaopick and Choose Eti nani wakuongea nae au wakumtembelea Ndani ya Bongo kisa eti wanajifanya wao ni Hadhi flani wanaishi kizungu Huwezi nipenda mimi wa Uk ukadharau watu wangu Wa Bongo. Pumbavu watu wamekaa ulaya na wazungu more than 15/20yrs na Bado wapo simple itakuwa wewe kibaka ulokuja kutembea au kikazi miezi 6 au mwaka mmoja kusoma?????!!! Wazungu wenyewe waishio kwao ulaya wapo simple. Basi hawa watu Trip hii ya Bongo nimewapa Fantastic Doze. Na wameshangaa hawakuamini nimewapotezea. Wenyewe wamejirudi. Hahahaaaaa. I love 2015.Jamanii mimi sishobokei mtuuuuuu hata uwe nani. I love simple real people . Genuine Individuals Only.# My wall My Voice.” Binafsi niliguswa na hiyo status nikajua kumbe si peke yangu ninaye sumbuliwa na watu kama hao, ilinipa faraja ndani ya moyo wangu. Na ndio maana leo nimeona ni vyema kuiwakilisha kwenu kama mada.

Shy-Rose-3
                                 Shy-Rose akiwa na mjomba wake pamoja na shangazi yake

Wazazi wanachangia sana katika hili swala. Unaweza kuta mtoto toka amezaliwa mpaka anakuwa mtu mzima hajawai kumuona bibi na babu walio wazaa wazazi wao,  hawajui shangazi wala mjomba eti kisa wanaishi kijijini. Nakama wapo mjini basi eti kwasababu wana hali duni basi hawana thamani kwao, kweli?  Tafakari!

One thought on “Ndugu ni ndugu tuu!”

Leave a Reply