Simplicity Is Always The Best

Shout out to my cute cousin-sister Lisa Makoyo. Kwa kweli si tu kapendeza bali uzuri wake wa asili na rangi yake ya chocolate inavutia sana.

FB_IMG_1428802177847Kuna baadhi ya wanawake ambao wanafikiria kupendeza ni lazima uvae nguo za expensive designers na upake poda, na marangi rangi mengi usoni,  kumbe wala si kweli. Hivi hujawahi ona watu wanavaa vitu vya pesa nyingi nabado wanaonekana “kituko” bara barani? Yani utakuta mtu kapaka heavy makeup, aye shadow za rangi za kung’aa, bangili, hereni yani makoro koro kibao usoni. Basi hapo ndo mkute ana nguo yake ya sijui designer gani na lipstick juu, ukimwangalia utazani yule ndege mwenye mdomo mrefu aitwae Kasuku!!

Halafu pia kupendeza siyo lazima uvae nguo za bei ya ghali. Kinachotakiwa kikubwa ni usafi wa mwili na mavazi. Unaweza ukavaa nguo yako uliyo ishona kwa fundi “Chochote” na bado ukapendeza zaidi ya yule aliye vaa nguo ya bei “chafu.” Kupendeza ni muhimu sana kwa kila mwanamke lakini kujiweka mapambo mengi inaonyesha kuwa ni mwanamke mwenye low-selfesteem (hujiamini).

Jamani kwa kifupi, simplicity is always the best, and too much of anything is harmful!! Tuige mfano wa Lisa Makoyo.

BTW, Black Girls Rock 🙂  🙂

Leave a Reply