Tazama unapo kwenda lakini kumbuka uliko toka

Kwakweli msema kweli ni mpenzi wa Mungu! Basi naomba niseme ukweli kuhusu huyu dada yetu Mh. Shy-Rose Bhanji kuwa ni mfano mzuri wa kuigwa kwa watu wengi hususani wadada. Wengi wanaweza wakawa wamemjua Shy-Rose sana baada ya kuwa mbunge wa Bunge la East Africa. Lakini ukweli ni kwamba dada yetu huyu alianza na kazi za kawaida kama Utangazaji katika kituo cha television cha TvT, pia na kwenye Bank fulani kabla ya kuwa Muheshimiwa!

Mh. Shy-Rose alipokuwa anasoma habari Televisheni ya 22/08/2014 Kamati ya uongozi EALA ilipotembelea IPP Media
22/08/2014 Kamati ya uongozi EALA ilipotembelea IPP Media

 Wapendwa, usiache watu wakukatize tamaa. Usiuwe ndoto zako eti kwasababu tuu fulani amesema huwezi, au amekataa kukusaidia. Piga moyo konde nyanyua kichwa juu, huko ndiko fungu lako lipo, Anasubiri tuu muda muafaka ufike akudondoshee! Hata kama wewe ni mbeba mabox nakusihi beba hayo mabox kwa nguvu zako zote ila kila siku hakikisha unazipa uhai ndoto zako. Yani usije  uwa ndoto zako labda itokee Mungu ameamua kukupumzisha.

Pia tunapo barikiwa kufanikisha ndoto zetu tusisahau tulipo toka. Au kuanza kudharau na kudhihaki wale ambao bado ndoto zao hazijatimia. Tuwe wapenda maendeleo ya wenzetu, ili tubarikiwe zaidi lazima nasi tubariki wengine. Tuige mfano wa dada yetu hapo juu ambaye siku ya jana ali post hiyo picha aliyo ambatanisha na ujumbe huu “Imenikumbusha mbali nilipokuwa nasoma habari Televisheni ya Taifa-TvT 2000-2003…Hapa ilikuwa jana 22/08/2014 Kamati ya uongozi EALA ilipotembelea IPP Media!” Hongera sana Shy-Rose Bhanji.

Leave a Reply