Tunakuwa wema kwa watu baki, lakini majumbani ni shida!

Tunakua wema kwa watu baki, lakini majumbani mwetu hasa kwa watoto zetu shida tupu

Nilikuwa nikiwahi kazini, nikiwa natembea haraka haraka nikaparamiana na mtu ambaye sikuwa nikimfahamu ” kwa kujishusha na kwa ukarimu nikamwambia samahani sana ndugu yangu, sikukuona ndio maana nikakuparamia, nisamehe sana.” FB_IMG_1467435053811Nilikuwa mpole mno wakati nikimwambia hayo. Na alinielewa na kunisamehe. Nikaendelea na safari yangu.

Lakini nyumbani ilikuwa ni hadithi nyingine. Jioni ya siku ile wakati napika jikoni, binti yangu alikuwa nyuma yangu akiwa amesimama. Nilipogeuka nilimparamia na kumuangusha.

Nilimkaripia nakumwambia pumbavu sana sasa unakaa nyuma ili iweje, haya inuka na uondoke hapa upesi sitaki nikuone!

Aliinuka na kuondoka pale kwa huzuni huku akilia. Sikutambua ni kwa jinsi gani nilikuwa mkali kwake.

Usiku wakati nimelala usingizi haukunijia na nikaanza kuwa katika fikra nzito nikafikiri nikiwa nimekwaruzana na watu nisiowafahamu barabarani nakuwa mpole kwao na kuomba radhi, ila kwa mwanangu nimpendae nimemuangusha hata samahani sijamuomba zaidi nimemkaripia!

Nikiwa naendelea kuwaza hilo akili yangu ikanisukuma niende nikaangalie angalie jikoni, kwenda kuangalia nikakuta maua yakiwa chini sakafuni ni maua ambayo binti yangu aliyachuma na alitaka kunipa kwa kuni suprise.

Niliyakusanya yale maua vizuri na nikayaweka ktk muonekano wake na nikaelekea chumbani kwa binti yangu. Niliinama na kumuamsha “amka mwanangu, amka!” haya maua ulichuma kwa ajiki yangu?

Alitabasamu a kuniambia “nimeyaona nyumba ya jirani nikaomba nikate machache kwa sababu ni mazuri kama wewe mama yangu” hapo hapo nikamwambia “binti yangu samahani sana kwa nilivyokua mkali kwako baada ya kukuangusha, sikutakiwa kukukalipia” binti akaniambia “usijali mama yangu, hata hivyo nakupenda” nikamwambia nami nampenda na nimeyapenda maua. Nikamfunika vizuri na kumtakia usiku mwema.

Usiku ule mwanangu alifariki kwa kubanwa na pumu, niligundua hilo baada ya asubuhi kwenda kumuamsha awahi shule. Nililia mno! Mpaka leo sijamsahau mwanangu machungu mengi mno moyoni mwangu.

Huwa najiuliza ingekuwaje kama angefariki na kinyongo cha mimi kumkaripia siku ile? Ila ninachoshukuru Mungu nilitengeneza amani nae kwanza. Ndipo mwenyezi Mungu akamchukua.

Muhimu: 

Hivi unajua kama ukifa leo kampuni yako unayofanyia kazi wanaweza wakamweka mtu mwingine kwa kipíndi kifupi tu kwenye nafasi uliyoiacha wazi?

Lakini kupoteza mwanafamilia ni hasara kubwa na pengo halizibiki kamwe! Umeshajitathimini na kujiona ni jinsi gani unaetendea familia yako? Mke wako, watoto wako au wazazi wako. Najua unaweza ukawa umejisahau.

Jifunze kuwatendea mema wapendwa wako, isije kuwa majuto ni mjukuu. Na kumbuka vitu hutumiwa na watu hupendwa.

Neno “Ningejua” huja mwisho wa safari

Mungu atusaidie.

Source: Tweve Hezron Facebook page 

Leave a Reply