Ujana ni ufunguo ~~~~Dina Marios

               UJANA NI UFUNGUO 

Hakikisha hupotezi funguo yako na unaitumia kufungua milango sahihi. Ukicheza na funguo yako ukaipoteza au ukachanganya usijue ufungue wapi, ukifika uzeeni ndio utajua. Sasa hivi ndio wakati wa kutengeneza maisha yako na sio uzeeni. Ukiharibu sasa hivi baadae itakuwa ngumu kuanza upya umri utakuwa umeenda.

Kijana wa leo ishi ukiwa na ndoto na maono. Sio woote Lila wengi wanaishi hawajitumi. Kijana umeshakuwa mkubwa uanze kujitegemea lakini bado unakaa nyumbani unagombania ugali na wadogo zako. Mtoto wake kiume umeshakuwa elimu unayo lakini hutaki kujishughulisha huna dira wala malengo. Watoto wa kike wamebeba uzuri kama ndio deal ya kuishi maana hana elimu, hana kazi, hana biashara, hana analolijua. Elimu anayo lakini maarifa hana ila uzuri ndio aloubeba na kuupa thamani. Hajui uzuri hufifia na kupotea je hapo baadae utaishije wakati uzuri haupo? Umbo zuri limekongoroka?

Wengi badala ya kusoma wamekimbilia mahusiano kuolewa ili iwe shortcut ya maisha………mume atamuhudumia.Ndoa zenyewe zimewafanya waishi kama Wajane ilhali waume zao hawajafa. Mateso, vilio na maumivu kila siku unalia wewe kama sio mjane kitu gani?? Simama usipoteze funguo yako……..kuwa na ndoto.

Kuwa na malengo na misimamo sasa hivi hakuna mwanaume anataka kuoa mwanamke mbugila mbugila. Huna mipango,huna maarifa wala mikakati. Unaamka saa tano hujui kupika wala kufua unajua vipindi vyote vya tv huna unachojishughulisha nacho, huna unalolijua upo upo tu. Kijana wa kiume huna ndoto zozote wala hujui unataka kuwa nani? baadae unataka uwe mume na baba wa familia kweli??? funguo yako unaijua kweli? unayo?

Kijana ishi kwa ujanja,uadilifu,kwa maarifa,kwa busara,kwa kujitambua na kwa tahadhari.
Dina Marios

Leave a Reply