Ujumbe wangu kwa Maria Sarungi-Tsehai

fb_img_1472436063790Siku ya jana kama ilivyo kawaida yangu nilipita huko Facebook kuangalia ni nini cha ku-share nanyi siku ya leo. Basi nikakutana na huu mjadala ambao mpaka muda huu nawaletea bado muhusika hajatoa majibu au kutoa ufafanuzi wa kutetea alichokisema. Hivyo sijajua kama ameona hamna haja ya kutoa maelezo zaidi au hakuona maoni ya mmoja wa mashabiki zake!……..Embu soma kwanza hiyo status iliyo andikwa na Maria Sarungi-Tsehai na pia usome maoni ya kaka Tommy kabla ujasoma mtazamo wangu!
img_20160916_085301fb_img_1472436063790Mmmh! Labda nianze kwa kusema kuwa ni kweli nakubaliana na Maria kuwa maisha ni “safari”! Lakini kitu amabacho Maria ameshindwa kuelezea watu ni kuwa hii safari ya maisha kila mtu ana yake kama ilivyo kwa safari nyingine! Kila mtu alikuja dunia kwa suku yake, muda wake, na ataondoka hapa duniani kivyake! Hatukuja wote siku moja hivyo safari zetu haziwezi fanana hata siku moja!

Kama zilivyo safari zingine watu ujiandaa na kubeba vitu tofauti wanapo safiri. Ndivyo ilivyo safari ya maisha yetu hapa duniani katika kile tunacho amini kukimbilia kama our destiny! Huwezi hata siku moja kulinganisha safari ya mtu aliye pitia maisha ya unyanyasaji wakati wa utoto wake na wewe ambaye umeishi maisha ya upendo siku zote! Safari ya mtu ambeye ni victim of child abuse ni tofauti sana na yako wewe Maria kwani huyu mwingine anasafiri na mzigo mkubwa mgongoni kwake ambao teyari ni kikwazo cha yeye kufika katika safari yake akiwa salama bila kukata tamaa na kwa speed ambayo wewe unaenda nayo!

Safari yako wewe Maria haiwezi kufanana na mtoto aliye zaliwa kwenye mazingira duni “uswahilini”! Ambapo wazazi wake siyo tu hawakuwa na uwezo kifedha bali hata elimu ya maisha ya hii dunia hawana! Hivyo nakubaliana na Tommy kuwa hatuwezi wote kuwa wakwanza kwani hiyo siyo issue! Naomba uelewe kuwa sisemi kuwa ni dhambi kwa wewe kuzaliwa Masaki, kukulia Masaki, na kuishi Masaki! Hapana! Ila nilitegemea kwa elimu uliyonayo na exposure uliyonayo ungekuwa muelewa zaidi katika maswa haya ya kufikia malengo a.k.a “safari” kwani hakuna dhambi mtu kuwa wamwisho kufika! Ulichokisema kinaonyesha some sort of dharau kwa wengine ambao bado wapo safarini, ego, na ushamba fulani wa mawazo mgando! Napia inapingana na msg ambayo uliandika hivi karibuni. Soma ? Mwanariadha

Umesema “ukijaribu kuhama-hama njia kila wakati bila mpangilio utapata madhara” ??? Kwakweli imenibidi nicheke kwanza! Hivi, unajua hii miili yetu tunatofautiana?! Kuna watu wapo safarini ambao ni wagonjwa (iwe kifedha, maradhi ya kawaida ya mwili, psychological trauma, emotional abuse, au kiroho) hivyo saa nyingine inabidi wasimame bila kutegemea!! Unafahamu kuwa wanapo rudi kwenye bara bara kuna uwezekano mkubwa sana wasirudi kwenye the same line waliyokuwepo mwanzoni?!! Na mtu utajuaje kuwa hii bara bara ni nzuri kwangu au hapana bila kujaribu kupita?! Mbona Prof. Sarungi aliingia siasa?! Mbona wewe sasa unataka kuwa entrepreneur, wakati huo huo unataka kuwa mwana harakati, na bado mambo ya urembo umeshikilia? Tofauti yako wewe na hao wanao hama hama bara bara ni nini?! Siyo wote wamezaliwa Oysterbay kwenye bara bara za lami, mipangilio ya mitaa, na taa kubwa zikimulika wakati wagiza!! Inabidi wajaribu kila kitu kabla ya kujua nini ni wito wao katika hii dunia! 

Maria, najua ni ngumu sana kwako kuelewa hichi ninacho kiongelea kwani wewe huja experience maisha halisi ya mtoto wa “mlala hoi” wa Tanzania au mtoto wa “uswahili”! But my dear don’t only use your brain to think but use your heart as well! Try to be sensitive na hizi msg zenu nyie watoto wa “Masaki” haswa kama kweli nia yako ni ku-inspire people na kuwa mfano mzuri kwa jamii!! katika maisha kinacho jalisha ni uthubutu wa kuanza safari na si kuwa wa kwanza kufika. Hata kama itakuchukua mika mia moja as long as umejaribu na umefika that is all that matters! Siyo lazima kila mtu atembee au kuendesha safari yake kwa speed yako wewe ndio uone kuwa wapo kwenye njia salama! Acha watu watembee kwa speed ambayo wao wanaiweza. Wewe jukumu lako ni kuwahimiza wasikate tamaa na kuishia njiani na siyo kuwatupia maneno ya ukandamizaji wa kisaikologia!! Every ‘saint’ has a story to tell and who are you to judge!

Leave a Reply