Una Akiba ya kuishi wiki moja bila kufanya kazi??

Regrann from @joycekiriasuperwoman – Leo tuna Nguvu za kufanya kazi, na tunaishi kwa kutokana na kipato tunachopata baada ya kutumia Nguvu zetu… Ebu fikiria ukiumwa wiki bila kupiga kazi utaishije?? Una Akiba ya kuishi wiki moja bila kufanya kazi??? (Kitaalamu unatakiwa uwe na Akiba za kukuwezesha kuishi miezi Sita bila kufanya kazi endapo utapata tatizo lolote) Mimi nakuuliza wiki moja tuu ????  Okay… Tujiulize Kesho tutakapokuwa tumepoteza Nguvu za kufanya kazi tutaishi kwa kipato gani???

Kama watu tunaobinuka kutafuta mafanikio tukae tutafakari juu ya hatma zetu, tujiulize kwa Sasa tunaingiza kiasi gani, na Miaka 20 baadae tutakuwa tunaingiza kiasi gani….

Wanawake wengi hapa sisi ni wahanga… Kuishi bila budget na mikakati tunaongoza ??? tunaishi bila kuwa na mkakati wa kifedha madhubuti, Tunaishi kwa matumaini ya kufanikiwa kupitia waume zetu ?? na Matokeo Yake tunakumbwa na Changamoto kubwa sana ya umaskini …. .

Semina by @joel_nanauka

Nywele by @rosebrazilian .

Kwa udhamini wa @hc_sanitary_pads – #regrann

Leave a Reply