“Usikate tamaa” by MeTL

Leo tumezindua rasmi kempeni ya “Usikate Tamaa” fb_img_1474070235644 Kampeni hii ilizinduliwa na Mkurugenzi wa Masoko wa MeTL Bi Fatema Dewji-Jaffer.  “Usikate Tamaa” ni kampeni kuhusu utoaji wa matumaini kwa jamii kupitia simulizi za watu waliokuwa na kipindi kigumu na wakafanya vyema, simulizi hii ni kwa ajili ya maendeleo ya kijamii.

Chapa yetu inajitofautisha sana na wengine katika soko si kwa sababu ya kuuza soda tu bali ni ile imani yetu kwamba kwa kila tufanyacho tunabadili maisha ya watu wetu.

Katika kampeni hii hatukulenga tu kufanya biashara lakini, MeTL kupitia chapa yetu ya Mo tunataka kutengeneza hisia, tunataka wananchi wetu kuhamasika wakati wanakunywa vinywaji baridi vya Mo, tunataka vinywaji vyetu kuwapatia matumaini zaidi kuendelea kupambana licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali fb_img_1474070242848Na sisi katika MeTL kupitia chapa yetu ya Mo tunaheshimu huo uwezo wa kutokata tamaa ambao watu wanao bila wao kujua, tunataka kuheshimu hilo, tunataka kuwapa tunzo watu hawa wa kawaida, tunataka kuwapa sauti ili watu wengine wawaige, hilo ndilo hasa linalomanaanisha kampeni hii ya Usikate Tamaa, huu ni mwanzo tu lakini tuna mengi sana katika siku zijazofb_img_1474070250224Katika uzinduzi wa kampeni yetu tulipata fursa ya kusikia simulizi za msanii maarufu wa miziki Tanzania, Sheta. Alisimulia magumu na vikwazo aliyopitia mpaka kufikia mafanikio bila ya kukata tamaa

Leave a Reply