Wewe ni nani hata ucheke wengine?!

FB_IMG_1473428092899FB_IMG_1472436063790Mpendwa hii dunia ya Musa nenda nayo polepole eeh! Haihitaji ujuwaji wala kimbele mbele…….!! Nilishawahi kusema huko nyuma kuwa siku zote dharau maiti lakini si binadamu mwenye pumzi ya uhai toka kwa Mungu kwani ya Mungu mengi! Sasa wewe jifanye ndio mtaalamu wa kucheka watu kwa mapungufu waliyonayo au kwa hali yoyote ile ambayo wewe unaona kuwa siyo nzuri! Waswahili tunasema “Mungu hamtupi mja wake”! Ipo siku fimbo ya Mungu itakuchapa pasipo wewe kujua na hapo ndipo majuto huwa mjukuu! Heshimu, ombea na watakie kheri watu wote bila kujali hali zao kwani aliyekupa wewe ndiye aliye ninyima mimi! ………. Hapo ulipo hata kuumba sisimizi huwezi pamoja na udogo wake ule alionao lakini huwezi muumba! Sasa ni nini kinakupa kiburi na jeuri ya kucheka wenzako?? Wewe ni nani hata ucheke wengine?!………Tafakari, fanya mabadiliko!FB_IMG_1473433434855

Leave a Reply