Zamaradi Mketema: Sidhani kama nikikupa Laki itakusaidia zaidi ya hiki

@Regranned from @zamaradimketema - Ninapoongelea kufanya VITU VIDOGO katika hali ya UKUBWA maana yangu huwa ni hii. @porridge_point ameniinspire hata mimi, kwanza ni degree holder, na wasomi wengi huwa tunaona mawazo yao hata ya kibiashara huwa ni makubwamakubwa tu, ila huyu baada ya kukosa kazi ameamua kuuza UJI, biashara inayoonekana sio ya hadhi yake labda kutokana na elimu yake, ila hakuangalia hilo sababu aliifikiria kwa ukubwa, huenda sio ishu kuuza uji, ila jinsi anavyouza ndio kulikonivutia, kuna wauza uji wengi mitaani kwenye machupa, lakini yeye ameona AONGEZE THAMANI, ameamua kwenda extra mile na kuwa mbunifu kwa kuwa na hizo take away cups zinazofanya yeyote ajisikie hata fahari kubeba, na hata sehemu yake ya biashara ameifanya tofauti na jinsi wauza uji wengine wanavyojiachiaga.  Sidhani kama nikikupa Laki itakusaidia zaidi ya hiki, nimeona nikupe muda wangu ili kuelezea Dunia nini unachokifanya,na zaidi kuweka contact zako hapa huenda ikafungua njia zaidi kwako, nimeona anasambaza hata kwenye mikutano ya kiofisi mbali na watu kumfata, kwa watakaopenda kuwasiliana nae namba zake ni 0654 197952, swipe kuona picha zaidi ama mfollow ili kuangalia anachokifanya.  Hongera sana na MUNGU abariki juhudi zako mama - #regrann

Leave a Reply