Furaha na amani ya siku ya Muungano!

Nawatakieni furaha ma amani ya siku ya muungano kwa Watanzania wote wenye mapenzi mema na nchi yetu! Mungu azidi kitusaidia tudumishe amani na utulivu katika taifa. Najua nchi yetu inamatobo ambayo yanatakiwa kuwekewa viraka, lakini siamini kuwa nchi yetu imeharibika kiasi cha kutofaa tena! Nguzo yetu kuu ambayo tumejivunia siku zote hata katika magumu yote tuliyopotia ni kulinda amani na umoja katika nchi yetu ndio maana marehemu baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere aliweza kuwaondoa wakoloni bila kumwaga damu! Kwani amani na umoja ndio alitaka uwe msingi wa taifa letu! Tujivunie amani yetu. Tushikamane sisi kama Watanzania bila kuruhusu kundi la watu wachache wenye nia zao potovu kuvuruga na kupoteza amani ya nchi yetu! Happy Union Day my beloved Tanzanians!

Mungu ibariki Tanzania. Mungu ibariki Africa.

Leave a Reply