Kesha la asubuhi: Muda U Karibu wa Kuondoka kwa Roho

             *KESHA LA ASUBUHI*
           JUMATANO MEI 30, 2018
      *Muda U Karibu wa Kuondoka 
                       kwa Roho*Na Roho na Bibi-arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure. Ufunuo 22:17.

? Kipindi cha rehema hakitaendelea kwa muda mrefu zaidi. Sasa Mungu anaondoa mkono wake unaozuia kutoka katika dunia. Kwa muda mrefu amekuwa akizungumza na wanaume na wanawake kupitia katika uwakala wa Roho Mtakatifu wake; lakini hawajasikia wito huu. Sasa anazungumza na watu wake, na kwa ulimwengu, kwa hukumu zake. Muda wa hukumu hizi ni muda wa rehema kwa wale ambao bado hawajapata fursa ya kujifunza ukweli ni nini. Kwa upole Bwana atawatazama. Moyo wake wa rehema unaguswa; mkono wake bado umenyoshwa ili kuokoa. Watu wengi watapokelewa katika zizi lenye usalama ambao katika siku hizi za mwisho watausikia ukweli kwa mara ya kwanza.

? Bwana anawaita wale wanaomwamini kuwa watendakazi pamoja na yeye. Wakati maisha yangalipo, hawapaswi kujisikia kuwa kazi yao imekwisha. Je tutaruhusu ishara za mwisho wa wakati kutimizwa pasipo kuwaambia watu kuhusu kile kinachoujia ulimwengu? Je tutawaruhusu waende chini gizani bila kuwa tumewasisitizia hitaji la matayarisho ya kukutana na Bwana wao? Isipokuwa sisi wenyewe tumetenda wajibu wetu kwa wale wanaotuzunguka, siku ya Mungu itakuja juu yetu kama mwivi. Machafuko yameujaza ulimwengu, na hofu kuu iko karibu kuja juu ya wanadamu. Mwisho uko karibu sana. Sisi tunaoufahamu ukweli tunapaswa kuwa tunajitayarisha kwa ajili ya kile ambacho kiko karibu sana kuujia ulimwengu kama mshangao wa ajabu mno.

? Kama kanisa ni lazima tuweke tayari njia kwa ajili ya Bwana, chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu. Injili inapaswa kutangazwa katika usafi wake. Kijito cha maji ya uzima kinapaswa kuongeza kina na kupanuka katika mwendo wake. Katika viwanja vya karibu na vya mbali, watu wataitwa kuacha plau-majembe ya kukokotwa na wanyama, na kutoka katika kazi za kawaida za biashara, na wataelimishwa pamoja na watu wale wenye uzoefu. Kadiri wanavyojifunza kufanya kazi kwa ufanisi, watatangaza ukweli kwa nguvu. Kupitia katika utendaji wa ajabu kabisa wa majaliwa ya Mungu, milima ya magumu itaondolewa.

? Ujumbe wenye maana sana kwa wakazi walioko juu ya dunia utasikika na kueleweka. Watu watafahamu ukweli ni nini. Mbele, na mbele zaidi, kazi itaendelea, hadi dunia yote itakapokuwa imeonywa. Na ndipo mwisho utakapokuja. -Review and Herald, Nov. 22, 1906.

*MUNGU AKUBARIKI*

Leave a Reply