Usikate tamaa!

Katika maisha watu tunapitia shida tofauti, na kila mtu ana kikomo cha uvumilivu wake. Lakini siku ya leo ningependa kuwasihii wapenzi wasomaji kuwa usikate tamaa. Mimi kuishi kwangu hapa Marekani kumenifanya nijuwe aina tofauti ya watu, nani ni rafiki wa kweli, na nani mwenye mapenzi ya dhati na maisha yangu. Pia imenifanya nijuwe uwezo wa kiwango cha uvumilivu wangu.

Katika hii dunia kuna watu watakuchukia kwasababu tuu ya mambo waliyo sikia fulani akisema juu yako bila hata yakuwa na huwakika nayo wawo tayari wanakuhukumu na kujenga chuki nawe. Wengine watakuchukia kwasababu zao binafsi ambazo hakuna mtu anaweza jua. Yani hata yeye ukimuliza kwanini anakukuchukia huwa hana jibu. Na wenigne watakuchukia kwa sababu chuki ni asili yao. Mimi katika changamoto ambazo nimepitia nimekutana na watu kama hao.

Sisemi kama nirahisi kuweza kujua nani ni nani mpaka uwe umechangamana nao. Nakama wewe ni mtu rahisi kama mimi kuamini watu kwa 100% kwa siku ya kwanza basi inakuwa ngumu zaidi kujua mpaka jambo litokee. Usikate tamaa. Kama unajua kuwa huko sahii naunacho kifanya, na unaamini kuwa yasemwayo ni chuki binafsi, basi wewe jiweke pembeni, mwachie Mungu.

Watu wengi wanaogopa kufanya maamuzi magumu, haswa inapo tokea wale wanao kuchukia ni watu wakaribu yako ambao walitakiwa kuwa ndiyo ngao yako. Naomba ukumbuke kuwa sanyingine mtu baki anaweza kuwa wa maana kwako kuliko hata ndugu zako wa damu, na nabii huwa hakubaliki nyumbani. Hivyo wewe fanya kile ambacho ni sahii kukifanya kwa wakati huo ili maisha yako yasonge mbele.

Samehe kadri uwezavyo, lakini usiruhusu watu wakugeuza wewe kanyagio la kufutia miguu yao michafu! Usifanye watu wafikirie kuwa wao ni Mungu; bila wao maisha yako hayato kwenda mbele. Hapana! Mungu pekee ndiye mtoaji wa riziki hapa duania, na huzigawa kutokana na wakati ambao Yeye anaona niwakati muafaka. Hivyo wakati wako ukifika wa kukubariki basi utapata fungu lako.

Mwisho, amini kuwa siku zote hauitaji kijiji kilicho jaa watu, au bank account iliyo jaa pesa ili wewe  uwe na furaha. Kuna watu wanapesa nyingi sana lakini hawana amani ndani ya nyoyo zao. Kuna watu wana utitiri wa marafiki lakini bado niwapweke sana ndani ya nafsi zao. Jitahidi siku zote uzungukwe na watu wenye mapenzi ya kweli na wewe.  Wale ambo wanapenda kukuona ukiwa na furaha wakati wote. Wale ndugu na marafiki ambao hawato kucheka ukijikwaa  katika maisha. Nakama ikabidi ubaki mwenyewe; basi nivyema zaidi kuliko kuzungukwa na watu walio jaa chuki na fitina. Usikate Tamaa!

The strongest man in the world is he who stands most alone.-Henrik Ibsen

  Mwamdishi wa Mada Hii
Mwamdishi wa Mada Hii

One thought on “Usikate tamaa!”

Leave a Reply