Usiamini katika wakati

Usiamini katika  Wakati kwani Wakati waweza kukudanganya… Wakati waweza kukufanya ukawa mpumbavu… Wakati waweza kukurudisha nyuma… Wakati waweza kukufungia milango ya Baraka…. Wakati waweza kukupotezea muda….

Usiamini kwamba ukiishi na MTU miaka 20 ukampa moyo  na mwili wako wote ukaongeza na maini na wakati wako wote basi ndio wako milele na hatakutenda….

Usiamini ukimzalisha /ukimzalia watoto 10 ndio wako wa maisha… Na Hata akikunyanyasa na kukutenda uendelee kumpa muda na kumuamini ukiamini atabadilika….

Usiamini katika  wakati kwani wakati hauna fursa… Binadamu tunazo fursa…. Usiamini katika wakati kwani wakati haufi… Binadamu tunakufa… Usiamini katika  wakati kwani wakati hauzeeki… Binadamu tunazeeka (japo najua wengi hatupendi uzee?)…

Usiamini katika  Wakati… KAMATA FURSA pale ulipo… Usiamini katika  wakati LIVE YOUR LIFE we just live once…. Usiamini katika  wakati JIAMINI MWENYEWE…..FB_IMG_1459686079711-2

Leave a Reply