Autism is not a disease, it’s a condition!

FB_IMG_1459863091911Kwanza naomba nianze kwa kumpongeza sana wifi yangu Veneranda Obure na binamu yangu Dr. Joseph Obure pamoja na wazazi wote wenye watoto wanao sumbuliwa na Autism inchini Tanzania kwa ujasiri wao wa kuweza kutoka mbele ya public na kueleza dunia kuwa watoto wao wanasumbuliwa na ugonjwa ujulikana kama Autism. Sio wazazi wengi wanaweza kujitokeza hadharani namna hii kwasababu ya kuogopa kauli za watu na stigma zao zilizo jaa ufinyu wa fikra!! Hongereni sana.

Nakumbuka mara ya mwisho nilipokuwa nyumbani. Rafiki / jirani yetu wa zamani alinisihi sana kuwa nisiondoke bila kumuona. Basi nami nilifanikiwa kwenda kuwasalimia. Katika kuongea ndipo akaamua ku-share nasi (nilikuwa na mdogo wangu Magreth) kuwa kwa muda mrefu ameangaika na mwanae na alipo mpeleka Nairobi kwa uchunguzi zaidi, doctor akamwambia kuwa mtoto wako ni autistic! Yani kwa Africa huu ugonjwa ndiyo sasa hivi wanaanza kuelewa tofauti na nchi zilizo endelea. Hivyo doctor akikwambia kitu kama hicho kwakweli kwa mzazi inakuwa ngumu sana kuelewa na hujui jinsi gani uchukulie. Hivyo nikitu ambacho rafiki yangu huyu kimemuadhiri sana. Na matatizo yanaongezeka zaidi haswa pale mzazi mmoja anapo kuwa hatoi ushirikiano katika kumuangalia mtoto.

Naomba Mungu ampe nguvu huyu rafiki yangu ili siku moja naye awe jasiri zaidi ya alivyo sasa, aweze kutoka mbele za watu na kushiriki na wazazi wenzie ambao wana watoto wanao sumbuliwa na Autism.                                            FB_IMG_1459863073585What is Autism!

FB_IMG_1459863122667Kuna huyu mwana mama ajulikanaye kama Holly Robinson Peete yeye ni mmoja wa wamama ambao watoto wao wana  sumbuliwa na Autism. Kwakweli napenda sana jinsi wanavyo handle hii situation ampaka imemsaidia sana ukuwaji wa mtoto wao tofauti kabisa na doctors walivyo sema. Na kitu cha kwanza wanasema ni wazazi kukubaliana na hali halisi. Halafu kuweza kuwa wazi kwa mtoto toka akiwa mdogo. (Tazama baadhi ya video ?)  

FB_IMG_1459863103016Mungu akinijalia uzima mwakani nitashiriki nanyi katika movement hii. I will walk for my darling nephew, mtoto wa rafiki yangu, na kwaajili ya watoto wengine wote wanao sumbuliwa na Autism hapa duniani. Mungu awape mwangaza doctors wanaofanya uchunguzi juu ya ugonjwa huu waweze kupata tiba haraka ?

Leave a Reply