ADUI WA TANZANIA NI WATANZANIA WENYEWE-Peter Sarungi

Peter Sarungi (Next Speaker-Baba Pilato)
Peter Sarungi (Next Speaker-Baba Pilato)

Inapotokea jambo fulani halifanyiki kwa mafanikio yaliyo tarajiwa basi wahusika hukaa na kutafakari ni kwa sababu gani jambo halijafanikiwa yaani maana yake wanatafuta mchawi ama adui aliye zuia mafanikio yao.

Tanzania yetu ni nchi yenye mipango mingi na mizuri na yenye kuvutia utekelezaji, nchi nyingi zimekuwa zikiiga mipango hii na kufanikiwa katika utekelezaji wake hata kuwa mfano kwa jamii za kimataifa. Chakushangaza ni pale unapo ambiwa kuwa chanzo cha mafanikio hayo ni mipingo iliyo buniwa na wataalaam kutoka Tanzania, maana utakuta utekelezaji wa mipango hiyo katika nchi ya Tanzania haiendani na wenzetu walio copy na kupaste kwao. Kwetu Tanzania utekelezaji umekuwa ni wa hasi na kuzalisha matokeo hasi kwa nchi.

Tumekuwa tukipata sera nyingi na nzuri lakini inapofika utekelezaji wake wanaibuka wana siasa wenye nguvu kikatiba kuliko watendaji na wanavuruga kabisa ule mpango kwa kuweka siasa katika utendaji na mwisho wa siku mambo yakiharibika wanasiasa wana ruka lawama na kuwasukumia rungu watendaji. Kila kitu katika nchi yetu kina endeshwa na siasa maji taka au siasa propaganda. Kuna haja ya wana siasa wetu kubadilika.

?????????? Hii ni shule niliyoikuta maeneo ya ndani ya Dodoma-Kibakwe katika jimbo la waziri wa TAMISEMI anaye simamia mipango na kampeni ya madawati katika shule zetu.fb_img_1481212567254Mmmmmmmh! ??????- Alpha

Leave a Reply