BAADHI YA VITU HATARISHI KWA NDOA YAKO – VIEPUKE

 

1. Gubu, tabia ya kuongea sana kwenye kitu kimoja, kulalamika na kulaumu mara kwa mara. Hii inaua sana intimacy
2. Tabia ya kupinga kila kitu, kuona kila afanyacho au apendekezacho mwenzako kinakasoro isipokuwa kile chakwako tu.
3. Ukali, ukatili na ubinafsi
4. Tabia ya kutafuta logic kwenye kila kitu, wewe kila analosema mwenzako unasema halina logic, fahamu sio kilakitu kwenye maisha ya mahusiano kina logic unayoijua wewe. Viko vingi sana vinahitaji uelewa tu. Just understand
5. Kutomsikiliza mwenzako, kila wakati kukwepa ukweli na uhalisia wa mambo
6. Kufanya maamuzi ya muhimu pasipo kumshirikisha mwenzako
Kwa kujiepusha na mambo haya utakuwa umeepusha kwakiasi kikubwa sana uwezekano wa ndoa au mahusiano yako kuharibika fb_img_1474555624518-1#ChrisMauki

Leave a Reply