Birthday wishes

2015-07-24 12.25.11Happy birthday to my most beautiful babysister Leonida Kachare! Mungu akubariki sanaaaaaa mdogo wangu wewe pamoja na familia yako yote.  Furaha, amani na upendo vidumu katika nyumba yako. Happy birthday girl love you mingi mingi ?

Wapendwa naomba mniruhusu niseme machache kuhusu huyu mdogo wangu. Namwita mdogo wangu si kwamba tuna undugu wa damu au ukoo mmoja hapana! Sisi ni ndugu ambao tumeunganishwa kwa ‘neema ya Yesu!’ Yani undugu wetu umetokana na jinsi family zetu tulivyo ishi!

Familia ya Mzee Kachare ni familia ambayo ukitaka kuongelea mafanikio ya wazazi wangu basi huwezi kuacha kuongelea familia hii! Kwani ina mkono wa baraka zake kwa familia yetu. Hivyo kwa namna hiyo tukajiona kuwa sisi sio majirani tuu, na wala si marafiki tuu, bali ni ndungu moja! Hivyo Leonida ni mdogo wangu kwa njia hiyo. Japo vile vile nao wanatoka Rorya, pande zile za Shirati nasi tunatoka Rorya pande za Utegi hivyo sisi bado wamoja.

Huyu mdogo wangu si mzuri tuu wa sura bali hata tabia na roho yake! Yani huwa saa nyingine ana m-surprise mama yangu nyumbani na mikungu ya ndizi, mara madebe ya mafuta tena yale mazuri ya bei ya ghali 🙂 na saa nyingine ana mletea mama yangu vitenge vya wax tena on Mother’s Day! Anatoka kwakwe anakuja kwa mama yangu kumuona. Siku zote huwa haendagi mikono mitupu “mama nimekuja kukuona mara moja maana ni muda sana mama yangu” hahaha!Yani hapo kama imepita miezi kadhaa hawajaonana na mama yangu. Yani anampenda na kumjali mama yangu kama ambavyo anamjali mama yake mzazi! Btw, mama yake mzazi na mama yangu ni wajina wote wanaitwa Cecilia! Sema mmoja ni mzaliwa wa Tabora na mingine ni mzaliwa wa Mara.

Anyway, Happy birthday beautiful, enjoy your day!

 

Leave a Reply