Busara za marehemu baba wa taifa

 2015-05-13 22.34.23“Hapa hatuchagui mtu maarufu, Hapa tunachagua mtu safi na huyu si safi. Kama unapenda sura yake basi nenda kanywe naye chai.  Wengine mnasema aaah ni tuhuma tu. Samuel (Sitta)! Yusuf (Makamba)! Mnasimama hapa mnasema ni tuhuma  tu! Lakini mtakumbuka mke wa Kaisari alipotuhumiwa  kwa ugoni Kaisari  akaagiza uchunguzi ufanyike. Uchunguzi ukafanyika na ikabainika kwamba sio kweli. Lakini Kaisari bado akamuacha, akasema mke wa Kaisari hapaswi hata kutuhumiwa. Na sisi hapa Mgombea wetu hapaswi hata kutuhumiwa wakati wapo wengine safi ambao hawana tuhuma. Kama mkimteua huyo mimi sitapiga kampeni. Siko tayari kumsafisha mtu matope  halafu ndio nimuombee kura. Hapana kabisa. Huyu mimi najua si msafi na nchi nzima inajuasi msafi. Hafai kuwa mgombea wetu.”  – Mwl. Julius Nyerere, NEC Dodoma, Juni 1995 Nyerere,

Credit to www.U-turn.co.tz

 

 

Leave a Reply