“Don’t make marriage a jail”~~~ChrisMauki

Enyi waume, wake zenu pia ni wanadamu, they are social beings, walikuwa na marafiki kabla hamjawaoa, usidhani wewe ndio ulikuwa binadamu wakwanza kwenye maisha yake. Kasoma kuanzia shule ya awali hadi chuo kote ana marafiki au hatakama hajasoma lakini ana marafiki wa mtaani na ujanani. Iweje leo kaolewa na wewe ndio unajifanya kumfungia kila mwanya wa kuonana na marafiki zake (simaanishi marafiki wa mapenzi), unamkataza kutoka, akienda vikao vya kinamama ni shida, akijiunga vikoba ni shida, akitaka kwenda kwenye mikutano ya dini ni shida kubwa, unamyima kuwa na marafiki na akitoka kidogo basi hauishi kupiga simu kumuuliza anarudi sangapi. Ikifika saa 12 jioni utaskia mwanaume anamwaga povu “wemwanamke uko wapi, wehujui ni mke wamtu? Unafanya nini nje hadi sahizi”? Mimi nikuulize, kwani wewe haujui kuwa wewe ni mume wamtu na baba wa watu? Sasita usiku unafanya nini nje ya nyumba? Au umekuwa jambazi? Simaanishi akichelewa asiulizwe la hasha, namaanisha kunyimwa uhuru kusipitilize ikawa utumwa, kisa eti wewe haupendi awe na mahusiano na wengine. Mwanamke hajaolewa na wewe kuja kuua ulimwengu aliowahi kuwa nao awali. Lets be fair to each other. Ni vizuri kilammoja akijali hisia na wellbeing ya mwenzake, na hapo ndipo furaha ya kuishi pamoja inapokuja. Dont make marriage a jail #ChrisMauki

Leave a Reply