Family ni msingi wa kila kitu ufanyacho!

 
           Kuna wakati familia huwa inaamua kukutana kwasababu tu wamejisikia kukutana. Saa nyingine mnajikuta wote mmetembelea eneo moja kwa wakati mmoja bila kujua hivyo mnakuwa mmekutana bila kukusudia. Mida mwingine familia inakuwa imekutana kwasababu kuna sababu maalumu ambayo inawalazimu wote kuwepo. Basi ndivyo ilivyokuwa hapa kwa familia ya mama na baba yangu. Walikutana kwa sababu maalum japo kwa leo sitaweza sema ni sababu gani iliyowakutanisha, hivyo wewe endelea kufurahia picha na pia endelea kutembelea blog hii kwani siku si nyingi nitakwambia ni kwanini family hii ya Mzee O.O Igogo iliamua kukutanisha ndugu zao siku ya jana Sunday July 8th, 2018.  Najua nawe utafurahia nami siku hiyo! 

Familia ni kitu ambacho kinathamani kuliko dhahabu na lulu. Ukiona mtu hajali familia yake au anapenda marafiki zaidi ya familia basi jua kunatatizo kubwa kwa akili yake!! Maamuzi ambayo tunafanya kila siku kwenye maisha yetu yanategemea sana tena sana nanfamilia tulizo kulia. Siku zote tupende na kujali familia zetu kwani ni hekalu dogo la Mungu.Hawa ni wadogo zangu wote. Msiwaone hapa wamekuwa wakubwa nimewaogesha na wengine nimewabadilisha nepi ? walikuwa wanaitwa "Bomoa group" yani ukipika "mahanjumati" lazima upike vya nyongeza maana hawafanyagi utani kwenye maakuli ?
 Hawa ni mashosti wa miaka mingi sana wamekuwa kama madada wa tumbo moja.Mungu ibariki hii familia na familia zote duniani katika jina la Yesu ??

Leave a Reply