Gone but not forgotten!

Mimi na kaka yangu (R.I.P) nyumbani kwa baba yetu mdogo-2010
Mimi na kaka yangu (R.I.P) nyumbani kwa baba yetu mdogo Segerea, TZ-2010

Wapendwa wasomaji wangu, naomba mniwiye radhi kwa mara ya kwanza na ya mwisho nitaongelea kuhusu kumbukumbu ya ndugu zangu na marafiki zangu ambao wamelala kwa amani ya Bwana. Siku kama ya leo miaka 4 iliyopita nilifiwa na kaka yangu kipenzi aitwaye William Charles Igogo au kwa majina mengine ni Mzee William au Jeshi. Yeye alipewa jina la marehemu babu yetu mzaa baba zetu (William Olung’a Igogo). Kwa heshima ya jina la babu vijana wote waliopewa jina la babu tunawaita Mzee William  (Sir William ) na kwakuwa babu alikuwa anapenda bunduki basi alipewa jina la “Ja jeshi”! Maana yake ‘mtu wa jeshini’. Hivyo huyu kaka yangu tulimkatisha na kumuita Jeshi. Na ndio jina ambalo alikuwa akijulikana nao sana kwa sisi wa nyumbani. Na kwa marafiki zake wa shule walimjua kama Willy  (William).

Marehemu William Charles Igogo a.k.a Jeshi

Nimesema nitaongelea kuhusu kumbukumbu za ndugu zangu na marafiki zangu ambao wamelala kwa amani ya Bwana leo kwa mara ya kwanza na ya mwisho kwasababu moja kuu. Mimi nimeamua ku celebrate life! Katika maisha yangu nimefiwa na watu ambao walikua si tuu muhimu kwangu bali pia walikuwa karibu sana na mimi. Vifo vyao vimeniachia pengo kubwa sana na maisha yangu will never be the same again! Kifo cha huyu kaka yangu mpendwa ndicho kilinifanya nifanye maamuzi hayo kuwa nitalia na kuhuzunika lakini sito omboleza milele! Na njia pekee ya mimi kuweza ku overcome the pain ni kuto sherekea kumbukumbu ya vifo vyao! Nitakuwa nikiwakumbuka kwa good memories we shared together in any other regular day (s) lakini nisingependa to bring the memories of their death days into life. Nashukuru Mungu kuwa watu ambao walikua karibu nami awe ni ndugu au rafiki nilihakikisha wanajua jinsi gani nawapenda na kuwa ni wamuhimu sana kwa maisha yangu. Kwakweli namshukuru sana Mungu kwa hilo kwani natumia kila nafasi ya uhai anayonipa kuhakikisha kuwa wale wanao gusa maisha yangu kwa njia moja au nyingine wanajua jinsi gani nawashukuru na kuwapenda. Na hivyo ndivyo nataka kuishi maisha yangu yaliyo baki. Basi, hamtaniona tena nikileta special post ya watu wangu waliyo tangulia mbele za haki………..Hii ? ni msg nyingine niliandika siku hiyo ya msiba. Na hiyo nyingine ni ya mdogo wake anaye mfuta ameandika leo. Kwa heshima na-share nanyi……………R.I.P brother and all my beloved relatives and friends ?   Screenshot_2016-03-21-19-50-49-1Screenshot_2016-03-21-20-55-18-1-1

2 thoughts on “Gone but not forgotten!”

  1. Pumzika kwa amani kipenzi chetu binamu. Sikumbuki kama tuliwai Kuwa mtu na binamu yake ila najuaga ulikuwa na nafasi ya kaka kwangu. Hata ktk maisha yako ya mwisho duniani hukutusahau. Ukatuchagua Kati ya wote nakumbuka simu yako usiku wa manane ukiniambia da tabu na binamu ma Maria nyie tu nataka muwe wasiri wangu. Ulimpenda kila mtu kwa nafasi yake ila mimi na wewe tuliambatana daima! Pumzika kwa amani

Leave a Reply