Hongera sana mjomba wangu Atanas Ageng’a

IMG-20150627-WA0000
Nimefurahi sana tena sana kuona mjomba wangu akipatiwa zawadi ya Bhajaji na Utegi Technical Enterprises (T) Ltd, hongera sana uncle Ageng’a! Ageng’a alipatiwa Bhajaji hiyo jana mjini Dar es salaam, Tanzania. Huyu mjomba wangu alishawahi kushiriki mbio za baiskeli za walemavu huko siku za nyuma naalibahatika kuutwaa ushindi kwa mara tatu kama kumbu kumbu zangu zipo sawa.

2015-06-27 23.32.50

Walio kuwepo hapo wakati watukio alikua Managing Director of Utegi Technical Enterprises (T) Ltd-Mrs. Magreth Mabada. Chairman and CEO wa Utegi Technical Enterprises na Saoligo Holding-Sir O.O Igogo.  Napia mfanyakazi wa Utegi Technical Sir. John Orwanda. Hongera sana Utegi Technical kwa kujali walemavu na watu wasio jiweza.

2015-06-27 23.31.23
Kwakweli huwa na furahishwa sana na urafiki ulipo kati ya huyu mjomba wangu na baba yangu mzazi, ni marafiki mmnooo! Huko siku za nyuma alisha wahi kumzawadia zawadi ambayo hata mimi siwezi sahau, ilikuwa ni siku ya harusi ya mjomba wangu na mkewe mpendwa. Kama tujuavyo nyumbani Tanzania kama wewe hali yako ni duni basi hata watu watakao hudhuria sherehe zako ni wale ambao hali zenu kifedha mnaendana nao; hivyo basi ni watu wachache sana walio kuwa wanajiweza kifedha au walio kuwa na hali nzuri kifedha ambao waliudhuria harusi yake, mmoja wao alikuwa baba na familia yake. Basi ilipo fika wakati wa kutoa mkono wa pongezi kwa maharusi baba yangu alim surprise kwa kuwapeleka honeymoon ya wiki nzima Bahari Beach Hotel. Yani miaka hiyo ya mwanzoni kabisa ya 90s hiyo ilikuwa a big deal! Kilikuwa nikitu ambacho kiligusa sana hisia za watu wengi sana walio kuwepo hapo hasa maharusi. Kwasababu hawakufikiria kabisa kitu kinaitwa honeymoon kwasababu ni kitu ambacho wahakuwa wanaweza kumudu gharama zake. Ukizingatia maisha yao yalikuwa ya hali ya chini sana na hapo harusi imefanyika Yombo vitu, achana na hii Yombo Vituka ambayo ina bara bara za lami naongelea ile Yombo Vituka ambayo ilikuwa na mapori ma mabonde 🙂 yani barabara ni vumbi, madimbwi tuu! Kwahiyo waweza pata picha ya maisha halisi walio kuwa wakiishi tena kwenye nyumba ya kupanga.

Anyway, hongera mjomba wangu furahia usafiri wako mpya. Mie penda wewe sana sana!

Leave a Reply