Je, unaishi mikononi mwa Farao?!

Kuna wakati unakuwa inlove lakini actuallywewe ni kama Mtumwa aliyeko Misri kwenye himaya ya Farao! Umekazana kulia na kumfurahisha mpenzi wako ambaye hana tofauti na Farao. Lina roho ngumu, hajali hisia zako, anaku-treat wewe kama object halafu wewe unavumilia na kupoteza muda wako wakati hata ndoa hujafunga naye! Wakati huku nje kuna akina Musa kibao wanajaribu kukutoa utumwani Misri ili uingie Kaanani, nchi ya ahadi, nchi yenye maziwa na asali, nchi iliyojaa upendo na furaha. Lakini wewe cha ajabu, unasema “you are in love?” na Farao?? Yani hupo teyari kufunga maktaba na shetani? Mateso yote anayokupa na kukutumikisha lakini you still think ipo siku life itabadilika na Farao atakuwa mwema! Farao hawezi kuwa mwema kamwe, hata siku Misri ibadilike haiwezi kuwa na Maziwa na Asali!!

Wake up, go after your destiny, toka Misri nenda Kaanani uishi kwa raha. Mapenzi yana raha sana ukiwa Kaanani, huyo Farao unaloling’ang’ania wala halikupendi na halina future na wewe. Poleni wale mnaodate na Farao, fungueni macho, Musa anawasubiri!!

Leave a Reply