Jokate Mwegelo: Namshukuru Mungu kwaajili ya wazazi wangu kwa kunilea katika maadili mema na hasa kunielekeza kwa Mungu na kunisisitizia elimu

Regrann from @jokatemwegelo - Miaka kadhaa iliyopita tarehe kama ya leo, taarifa zilienea Mama Kidoti amejifungua salama mtoto wa kike. Nilizaliwa kama watoto wengine wa kitanzania, wapo waliofurahia ujio wangu, na naamini wapo waliotamani ningekuwa mtoto wa kiume ?. Lakini Mwenyezi Mungu kwa hekima zake alinileta mwanamke. Hakuna aliyejua nimebeba nini ndani yangu kwa kuniangalia kwa macho, wala hakuna aliyejua nitakuja kuwa nani. Hayo yote Mungu aliyaficha katika hekima yake. Namshukuru Mungu kwaajili ya wazazi wangu kwa kunilea katika maadili mema na hasa kunielekeza kwa Mungu na kunisisitizia elimu, pia kuamini ndoto zangu, hata leo nimefika hapa nilipofika. Nawashukuru wote walioniamini na kuni-support hata wakati ambao mwenyewe sikujiamini katika ndoto kubwa nilizokuwa nazo. Naishukuru team yangu ya KIDOTI, partners wangu, na watanzania wote kwa ujumla kwa kuendelea kusimama na mimi kila hatua. Nakiri kwamba peke yangu nisingeweza kufanya chochote.
.
.
Ninayo furaha kubwa kuongeza mwaka katika maisha yangu hapa duniani, ni fursa ya kipekee kuwa hai. Wengi walikuwa na ndoto kubwa huenda kuliko zangu lakini hawapo nasi. Uhai ni zawadi na kwa hilo namshukuru Mungu. Maadam Mungu ameniacha hai ni ishara kuwa ana mipango mikubwa na maisha yangu ili niliishi kusudi lake na kutimiza kile aliniumba kufanya Tanzania na ulimwenguni kwa ujumla.

NI KWA NEEMA NINAISHI. HAPPY BIRTHDAY TO ME.
#KIDOTI #BIRTHDAYGIRL #KIDOTI2018 ?❤?? cc @rapture1913 @mkolikoli @cmagavilla ? - #regrann

Leave a Reply