Kesha la asubuhi: Heri wenye moyo safi; maana hao watamwona Mungu

*KESHA LA ASUBUHI*

ijumaa. *23/03/2018*

*Usafi*

?

*Heri wenye moyo safi; maana hao watamwona Mungu. Mathayo 5:8.* ??. Mtu akiwa ameondolewa ubinafsi kabisa, wakati kila mungu wa uongo anapoondolewa kutoka moyoni, ombwe hujazwa kwa mtiririko wa Roho wa Kristo. Mtu wa namna hiyo huwa anayo imani itendayo kazi kwa upendo na kusafisha moyo kutokana na kila uchafu wa kimaadili na kiroho. Roho Mtakatifu, Mfariji, anaweza kufanya kazi moyoni, akiweka mvuto na kuongoza, kiasi cha mtu huyo kufurahia mambo ya kiroho. Mtu huyo anakuwa “aifuataye Roho” (Warumi 8:5), naye huyafikiri mambo ya Roho. Huyu anakuwa haweki tumaini katika nafsi; Kristo ndiye yote katika yote. Bila kukoma, ukweli unakuwa ukifunguliwa na Roho Mtakatifu; naye hupokea kwa upole neno linalopandikizwa na kumpa Bwana utukufu wote, akisema, “Mungu ametufunulia sisi kwa Roho” (1 Wakorintho 2:10). “Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu” (aya 12).

??. Roho anayefunua pia hutenda kazi ndani yake katika kutoa matunda ya haki. Kristo anakuwa ndani yake, “chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele” (Yohana 4:14). Yeye ni tawi la Mzabibu wa Kweli nalo huzaa vishada vilivyosheheni vya matunda kwa utukufu wa Mungu. Matunda yanayozaliwa yana tabia gani? “Tunda la Roho ni upendo.” Zingatia maneno haya – upendo, siyo chuki; ni furaha, siyo hali ya kutoridhika na kuomboleza; amani, siyo harara, fadhaa, majaribu yaliyotengenezwa. Ni “uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria” (Wagalatia 5:22, 23).

?? Wale wenye Roho huyu watakuwa watendakazi wenye bidii pamoja na Mungu; wajumbe wa mbinguni watashirikiana nao na wanakwenda wakiwa na uzito wa Roho mwenye ujumbe wa kweli ambao wanaubeba. Hawa wanakuwa tamasha kwa ulimwengu, kwa malaika na kwa watu. Hawa wanakuwa wameadilishwa, wametakaswa, kupitia kwa utakaso wa Roho na imani ya ile kweli. Hawa hawajaleta kwenye hazina ya nafsi; kuni, majani, visiki, bali dhahabu, fedha na mawe ya thamani. Hawa hunena maneno yenye uzito wa maana na kutoka kwenye hazina za moyo huleta mambo safi na matakatifu kulingana na mfano wa Kristo. – Home Missionary, Nov. 1, 1893.

*tafakari... Njema*"""
.
.

Leave a Reply