Kheri ya kutimiza miaka 7 ya ndoa!

FB_IMG_1452148528820Wow! Nianzie wapi kusema mim Alpha! Ee Mungu Nipe busara na utulivu wa akili ninapo andika haya maneno ili nisisahau hata moja. Na yote nitakayo sema si kwaajili yangu mimi bali sifa na utukufu zote ni zako wewe uliye Mkuu! FB_IMG_1452150546873-1Naomba niwatakieni kheri ya kutimiza miaka 7 ya ndoa yenu Mr and Mrs Nyongo! Mungu azidi kuilinda ndoa yenu. Akaifunike kwa pendo lililo kuu! Upendo usio tikisika, upendo wa agape! Azidi bariki nyumba yenu na uzao wenu wote. Watoto wenu wakajae baraka, wawe nuru mbele yake yeye Mungu Mkuu na dunia nzima! Nashindwa niseme nini juu yenu kwani upendo na ukarimu mlio nipa mimi Alpha hauelezeki wala hausimuliki! Mimi ni nani hata mnitendee haya yote?! Lakini naamini palipo na Mungu siku zote kuna upendo wa kweli; nyinyi ni watu wa Mungu, mmemvaa Mungu ndani ya myoyo yenu na ndio maana upendo wenu kwa watu ni wakweli! Ee Baba Mungu bariki hii ndoa. Inapotimiza na kusherekea miaka 7 ya kudumu pamoja, kaa nao wadumu ndani yako na shetani asipate nafasi……Asanteni sana tena sana kwa ku share story yenu nasi. (Soma hapa). Happy 7th Wedding Anniversary to you and happy Valentine’s Day! I love you dearly! ❤❤❤

Leave a Reply