Linda Bezuidenhout machoni pangu mimi!

unnamed-2-1Wapendwa wasomaji wangu. Niliahidi wiki hii nitamzungumzia mwanamitindo wetu maarufu anayetamba katika anga za kimataifa Ms Linda Bezuidenhout. Napia nini msimamo wangu juu ya kile kinacho onekana kama maugomvi katika social media!  FB_IMG_1438787818246Naomba kwanza muelewa kuwa mambo ya campaign yameisha, sasa tunarudi katika maisha yetu yakawaida. Wakati wa campaign mimi na Linda tulikuwa tumesimama pande mbili tofauti. Linda yeye ni mwanachama mwaminifu wa Chadema a.k.a UKAWA  hivyo alikuwa anam-support Mr. Edward Lowassa kama mgombea urais kwa upande huo. Mimi nilikuwa na msupport Dr. John Pombe Magufuli kama mgombea urais. Lakini pamoja na kutofautiana kwetu hatujuwahi kutupiana maneno ya kashfa wala matusi. Wote tulipigia “debe” wagombea wetu huku tukiendelea kuheshimiana! Hivyo sina sababu yoyote ya mimi kutokuendelea kumpa support Linda kwa kazi zake anazo zifanya kwani nikitu ambacho nilikuwa nafanya siku zote! 11707864_709621275810853_6240265761321765145_nKunawatu walishawahi kutoa comment ya kuniuliza mbona kwenye interview zangu nilizofanya na Linda sijagusia ‘maugomvi’ ya Linda kwenye social media? Sikuwahi kujibu chochote lakini leo naomba nijibu kwa mara ya kwanza na ya mwisho!FB_IMG_1431701419254Siwezi kukataa kuwa hayo maugomvi hayapo kwani mie unafiki siuwezi! Ndio, maugomvi yapo lakini “mnyonge mnyongeni haki yake mpeni!” Kama nilivyo sema hapo mwanzo kuwa haya maugomvi yapo kwenye social media. Nakama tukiwa wakweli na waungwana basi tutakubali kuwa hata huko kwenye social media hayakufati kwenye profile / account yako! Ni vitu ambavyo lazima uvitafute wewe mwenye! Kwamfano mimi mwanzoni nilikuwa sijawahi yaona mpaka juzi juzi tuu nilipofungua IG account na kuamua kuyatafuta kwani niliona watu wakimtaja jina lake mahala fulani. Lakini kiukweli kama nisingeangaika kuyatafuta huko inamaana nisingeyaona! Hivyo mimi siwezi kujiingiza kwenye mambo  au maugomvi nisiyo yajua mwanzo wake wala mwisho wake! Nimejaribu kutafakari sana na kujiweka katika nafasi ya Linda nikajiuliza je ningekuwa mimi ningefanyaje?! Jibu langu ni SIJUI! Kwani kila mtu ana react tofauti na kila mtu anakiwango chake cha uvumilivu! Hivyo  who am I to judge anybody! Na haswa ukizingatia kuwa sijui nini kiini cha maugomvi yao! Pia ukizingatia kuwa hivi ni vitu ambavyo mtu mwenye uwamue kuvitafuta ndipo utakutana navyo lakini ukiamua kutokufuata hizo account / profile ukweli hutokaa ujuwe kuwa kuna ugomvi wowote! Labda niseme watu wa kulaumiwa ni nyie mnaofuata hayo maugomvi huko na kwakutumia account zenu zenye majina fake mnatukana na kuchochea maugomvi ambayo ukiulizwa unajua chanzo chake au yanakuhusu vipi hutokaa uwe na jibu!! Nyinyi wenye account fake ndio wa kulaumiwa na kulaaniwa vikali sana. Naomba Mungu awalipe kulingana na mnavyo stahili!! unnamed (1)Labda niwaelezee kidogo jinsi Linda alivyo macho pangu mimi Alpha Igogo!  Linda ni mtu mmoja muungwana sana, mkarimu, ana roho nzuri mno, mcheshi na mwenye upendo mwingi sana! Narudia kusema “mnyonge mnyongeni haki yake mpeni!” basi niacheni nimpe Linda haki yake kwani anastahili! FB_IMG_1428375240553Jamani jinsi mnavyo muona Linda alivyo mzuri wa sura na maumbile basi ndivyo alivyo na roho yake! ni watu wachache sanaaaaaa tena sanaaaaaa ambao wamebarikiwa kupata vyote kama Linda, yani uzuri wa sura na roho! 11236426_709423212497326_6576415971030545565_nLinda mnayemuona pamoja na familia yake walinikaribisha kwao na kuniudumia kana kwamba mimi ni mtoto wa mfalme fulani! Mimi na hii familia tulikuwa hatujuani wala hatujawahi kuongea hata siku moja. Walipewa utambulisho wangu na kaka yangu Dj Luke wa Vijimambo blog  lakini walivyo nipokea na kunihudumia utafikiri mtu ambaye wamenijua miaka nenda rudi. Tena hapa Marekani ambapo watu wengi hawapendi kukaribisha watu kwenye nyumba zao?! Lakini Linda na familia yake ikanikaribisha kwa moyo mkunjufu na kunifanya nijione kama sehemu ya familia yao! Halafu eti mimi leo watu mnataka nigeuze shingo yangu nakuitenga hii familia kisa na mkasa eti maugomvi ya kwenye social media ambayo siyajui mwanzo wala mwisho wake!! Tena maugomvi yenyewe mpaka uyatafute huko?! Jamani, si hata Mungu ataniadhibu!  FB_IMG_1437317045145Hivi mnajua ni jinsi gani inavyo uma unapo mkaribisha mtu kwako kwa moyo mweupe kabisa, mtu ambaye ulikuwa hata humjui, ukaacha kazi zako, ukachukua muda wako kumpikia, na kumu-entertain, na pia kuwapeleka kwenye hotel nzuri ya gharama kula nao dinner  halafu kesho yake unamuona ameungana na watu ambao umetofautiana nao kisa kakasirishwa na reaction yako?! Unajua huo ni unyama na moja ya ukatili wa hali ya juu?! Au kwasababu watu wengi si wakarimu ndio maana mnadiriki kuniuliza mimi nasimama wapi katika hili?! FB_IMG_1437317045145-1Don’t get me wrong, sishabikii hata siku moja maugomvi yanayo endelea kwenye social media za wabongo! Nalaani vikali mno! Lakini hivyo haviwezi kuniondolea utu wangu wakuthamini uungwana na ukarimu walionao hii familia! Nitakuwa mtu mbaya sana kama nitanyanyua mdomo wangu na kusema vibaya hii familia au kuungana na watu walio gombana nao kwasababu ya ushabiki tuu! Mimi sio NYUMBU! NAKATAA SITOFANYA HIVYO HATA MARA MOJA! Hivyo naamini mtaniacha mimi kama Alpha Igogo nisimame kama Alpha Igogo. Niendelee kuwa huru kuisupport na kupenda hii familia bila kipingamizi chochote! 11692730_709621169144197_3015601318729094842_nNaomba msiniuhusishe na kitu au ugomvi wowote hule ambao haunihusu! Sishabikii ugomvi wowote lakini napenda kusimamia ukweli.  Na ukweli ni kwamba Linda wala familia yake hawajawai kunikosea wala kunivunjia heshima, hivyo sitaki kuchuma dhambi na kujipa laana kwa vitu visivyo nihusu! 11659348_709620845810896_6802823800920420064_nLinda dada yangu, Mungu amekupa mume anaye kupenda kwa moyo wote. Naomba umuonee huruma huyu baba. Najua uliumia sana, lakini imetosha sasa, mpe mmeo heshima anayo stahili! Naomba dada yangu uachane na hayo maugomvi. Umepewa karama ya upendo ambayo wengi hawana lakini umefanya watu wameshindwa kuona karama yako ya ukarimu na upendo kwasababu ya haya maugomvi.   Screenshot_2015-12-08-15-18-36-1Nyinyi nyote mnaogombana ni watu wazima wenye familia zenu hivyo siwezi sema mengi kwani nyinyi wenyewe ndio mnamaamuzi ya mwisho ya nini kifanyike! Mimi nasema kama Alpha lakini muamuzi ni Linda mwenyewe na maamuzi yako nitayaheshimu sikuzote! 11541979_708046672634980_678590546258737464_nNafikiri ni wakati muafaka sasa wakuona si tuu Wamerekani wakivaa nguo zako bali watu walio au wanao heshimika katika taifa letu la Tanzania kama mama Janeth Magufuli  au kwakuwa wewe ni shabiki wa Chadema basi watu kama mama Regina Lowassa waanze kuvaa nguo zako kwani unastahili na unamapenzi sana na Tanzania. Lakini ninahuwakika kama utaendekeza haya maugomvi itakuwa ni ngumu sana kwao kukupa support yao. Kumbuka si kila mtu amepata nafasi ya kukujua kama mimi Alpha Igogo nilivyo kujua! Na si wote utakaowapa au uliowapa nafasi ya kukujua wanauwezo wa kusimamia ukweli! Watu walio wengi wanajali “reputation” zao katika macho ya watu, bila kujua character zao ndizo zitakazo  simama siku ya siku! Hivyo ni nadra sana kukuta watu wakasimama na wewe kwani wanahofia kuharibu reputation zao. 2015-06-22 20.21.51Natuamaini nimejieleza vya kutosha, wenye kunielewa watakuwa wamenielewa. Naambao hawatanielewa basi naomba tukubaliane kuto kukubaliana. Kila mmoja abaki na msimamo wake, muhimu tuheshimiane. Linda na familia yako, naomba nirudie kusema asante sana kwa ukarimu wenu Mungu azidi kuwalinda na kuwapa maisha marefu yenye amani, furaha, upendo, na afya njema.  Asante. 11012586_709423359163978_2611958792103710880_n

One thought on “Linda Bezuidenhout machoni pangu mimi!”

Leave a Reply