Mama Salma Kikwete umekosea sana! Hiyo inaitwa institutionalized discrimination!!

Sipendi kuongelea maswala ya siasa tena kwa hii blog ila kuna mambo ambayo nikiona kuna umuhimu wa kutoa maoni yangu basi nitafanya hivyo. Mama yangu mama Salma Kikwete unajua nakupenda sana. Jambo kuu katika sheria za upendo ni kumwambia mtu ukweli pale anapo kosea. Basi nami naomba nikwambie kuwa  mama yangu umekosea sana!

Nimesikiliza kwa makini hoja yako juu ya wanafunzi wanaopata MIMBA wakiwa mashuleni ikanigusa kwa masikitiko makubwa sana kwani huyo mwanafunzi ambaye wewe unamuongelea LEO alikuwa ni mimi MIAKA 23 iliyopita! Siamini leo hii baada ya miongo miwili kupita hili swala bado halijatafutiwa suluhisho chanya ndani ya Tanzania na leo hii inabidi nisimame kuwatetea waathirika wote wa mimba za utotoni/ mashuleni?!

Awali ya yote naomba utambuwe kuwa hakuna binti yoyote anayependa kupata mimba akiwa shule. Lakini hiyo haimaanishi kuwa wanaopata mimba ni wanadhambi kuliko wale ambao hawajapata mimba au wanaotoa mimba. Hii stigmatization na discrimination kwa wanafunzi wanaopata mimba au mabinti wanaopata mimba kwenye umri mdogo lazima jamii ikemee kwa nguvu zote. “Structured” life style ndio tatizo kubwa sana katika familia na jamii  nyingi za Kiafrika haswa Tanzania!!

Pili nani alisema mimba ni ugonjwa unaomzuiya binti kuendelea na masomo yake?!! Mnapo mzuiya huyu binti kuendelea na masomo yake vipi kuhusu mwanaume aliye mpa huyu binti mimba?! Yeye anapewa adhabu gani?? Kwanini watoto wakike ndio wamekuwa wa kubebeshwa lawama na mizigo yote bila kuangalia both sides of the coin?? Hivi hizi mimba huwa wanajipa wenyewe au?! Na vipi wale ambao wanapata mimba kwa njia ya ubakaji nao wapo kwenye hukumu hii au?!!

Mama yangu, umesema vitabu vyote vya dini Qur’an na Bible eti vinakataza watoto wa kike kupata mimba kabla ya wakati?! Ni wakati gani huo unao uongelea wewe?! Mimi sijui juu ya Qur’an lakini naelewa Bible takatifu inasema “waacheni watoto wote waje kwangu maana ufalme wa Mbingu ni wao” haikusema watoto waliozaliwa na mama wa umri gani wala katika mazingira gani!! Bible imekataza UZINZI tu! Na hilo ndio swala ambalo jamii yetu bado ipo kwenye koma ya mawazo mgando halitaki kuliongelea kinaga ubaga!!

Unaongelea mila na desturi za Mtanzania halafu unachanganya na Biblia?! Unajua hapo ndipo watu wengi wanapojichanganya! Kama mnataka kuongelea mila basi msimame na mila zenu bila kuingiza vitabu vya Mungu! Halafu muache kwenda kule Ukuryani na Umasaini kuwaambia waache kukeketa watoto wakike kwani hata wao wanafuata na kutunza mila zao!! Mnaongelea mimba za watoto washule na kuwahukumu kwa kutumia neno la Mungu, vipi wababa wanao zaa nje ya ndoa hao mnawapa adhabu gani? Vipi wanaume wa Kikristu  waliofunga ndoa na wana vimada nje au wameowa wake wawili wakati Biblia hairuhusu?!

Mama Salma, dunia yote sasa hivi inaongelea jinsi ya kumnyanyua mtoto wa kike ili aweze kupambana na maisha hata kama atakuwa amepata changamoto za aina gani, sasa wewe unataka kuzidi kuwakandamiza watoto wa kike kwa sababu ipi haswa?! Je, unajuwa waathirika wakubwa  wa hii institutionalized discrimination yako ambayo unaipigia debe ni wale watoto wanaotoka kwenye familia duni?! Kwasababu ninahuwakika nyie wanenu wana uwezo wa kwenda kupata vidonge vya mpango wa uzazi wakati wowote hivyo hawa wa wenzenu ndio mnawaona wadhambi sanaaaa!!

****ITAENDELEA……****

 

Leave a Reply