Mkutano wa wanajumuiya ya THC na Detective Todd Tyler

Siku ya Juma Mosi tarehe 21 May, 2016 majira ya saa kumi jioni (4pm), wanajumuiya ya THC walikusanyika na kumuuluza Todd Tyler (The Lead Detective of homicide case of Andrew Sanga) maswali ambayo walikuanayo juu ya nini kinacho endelea kuhusiana na case ya mpendwa ndugu yetu Andrew ‘Drew’ Nicky Sanga a.k.a King 404. Mkusanyiko huo ulifanyika kwenye makutano ya barabara ya De Moss Drive na Fondren ambapo ni sehemu marehemu alipigwa risasi…….. Watu wengi walijitokeza, bado hisia za watu zinahuzuni nyingi ambapo wengi walitaka kujua nini haswa kina endelea na wao kama jumuiya wafanye nini kusaidia kurahisisha na ku speed-up uchunguzi ili mtuhumiwa aweze kupewa adhabu anayo stahili. (Tazama videos ? part 1 & 2)

 Mkutano huo ulichukua zaidi ya masaa mawili kwani watu wengi walikuwa wanamaswali na Detective Tyler alikuwa yupo teyari kusikiliza na kujibu maswali yote. Kuna maswali ambayo yaliandikwa in advance kutoka kwa watu mbali mbali na kuna maswali ambayo yalijitokeza kwa wakati huo; na yote yalijibiwa kwa kuzingatia sheria na kanuni za upelelezi haswa za kesi za mauwaji!…….. Miongoni mwa watu walioudhuria mkutano huo nipamoja na mzazi mwenzie marehemu Andrew aitwaye Emmy pamoja na binti wa marehemu Zoe Sanga. Mkutano huo uliogozwa na Mwenyekiti/ President wa jumuiya ya Watanzania waishio Houston, Texas ndugu Mayocha

Naomba ifahamike kuwa hizi post ni zangu mwenyewe, hazijatoka kwa viongozi wa THC. Nime share nanyi kwa mapenzi yangu binafsi hivyo nipo fully responsible kwa chochote kile! Naomba niombe msamaha kama kuna mtu yoyote atakuwa amekwazikwa kwa hii post kwani hilo si lengo langu! ……… Poleni sana wafiwa wote, ndugu, jamaa, na marafiki!…….. Until the morning glory comes continue to rest in peace Andrew!

Leave a Reply