Harusi ya Mr & Mrs Huckins

received_10207244732468216-1

Neema naomba unisaidie kutafsiri kwa shemeji yangu, lugha za wenyewe ngumu #MimiMaimuna ??? …………..haya mabibi na mabwana hiyo ndiyo ilikuwa kadi ya mnuso kwa walio alikwa. 2016-02-01 09.05.03Jamani, walipendeza sana hata mwenyewe si unawaona?! Mtoto “cheusi mangala” toka Magu, Mwanza, Tanzania amefanikiwa kuuteka moyo wa “mzungu” kwa maisha ya umilele, simchezo! Lakini sifa na utukufu zote zimwendee Mungu wa Mbinguni ? received_10207249360143905-1hapa bibi harusi wetu akifanyiwa urembo wa mwisho mwisho na mpambaji anayechipukia na anakuja juu sana kutoka huko Atlanta, Georgia. Nitawaletea post juu yake ili mumjuwe ni nani. received_10207244742388464Binti yake Neema anamuangali mama yake kama kila kitu kipo sawa na yupo teyari kukutana na mfalme wa siku hiyo ambaye ni baba yake. Raha sana. Upendo wa dhati!received_10207244743508492?? anameremeta….anameremete….anawakawaa …..anawakawaka ??? ulipendeza sana Neema. Yani makeup zilikuwa za ukweli na nguo ilikukaa vizuri sanaaaaaa ?? received_10207244737308337-1Mrembo wetu akiwa na kaka yake kipenzi aitwaye Meki. Kwa upendo na furaha nyingi anamsindikiza dada yake na kukabidhi kwa shemeji yake Huckins. Ubarikiwe sana kaka Meki.received_10207244736788324-1Hapa naona bibi harusi wetu akionyesha tabasamu lenye furaha nafikiri ni baada ya kuona sura ya ‘mfalme’ wake ikimngojea kwa hamu nyingi. Vile vile ukimwangali kaka Meki utaona “kahuzuni” fulani usoni kwani ni zile saa za makabidhiano zimefika, na punde atakuwa si wakwao tena ?? received_10207244738188359-1To honor, to cherish, and to love; Yes I do! Alicho kiunganisha Mungu mwanadamu asikitenganishe! Ngoja niweke msisitizo, mnasikia nyie “wadada wa mujini” nyie “wazungu weusi” Ni hivi……… What God has joined together let no man put asunder!!  and let wasomaji wangu wote say Amen! received_10207244597704847It’s official! Mr and Mrs Huckins ????received_10207244593064731Ooh nakupenda  siyo siri nakuhusudu ooh ni wanguuu…….awwh! Too cute!received_10207244598424865-1wow! Neema ulipendeza sanaaaaaa! Nguo zuri, imekukaa vizuri sana, makeup safi kabisa. Mungu akuongoze ndoa yako idumu milele! received_10207244598024855Our “foreigner” shemeji ?? shemeji yetu wa kimataifa ati! Katoka kwa Obama mpaka Magu kwa ndugu zake na Dr. Magufuli kumchukua mrembo wetu na kufanya awe “pambo” la nyumba yake mpaka kifo kitakapo watenganisha. Jamani embu mpigie makofi na vigere gere vya nguvu popote pale ulipo shemeji yetu wa haja! ????????????  Welcome to Lake Zone Region our beloved brother in law! received_10207244598664871Jamani wamependeza sanaaaaaa! received_10207244735988304Watu wenye upendo wa kweli utawaona tuu, huwa wanafurahishwa na kupendezwa  na mambo ya wengine. Nyuso zao huwa na furaha kwenye shughuli za watu, si mnawaona hawa?!! Mbarikiwe sana wapendwa. received_10207244745628545Ukumbi umepambwa ukapambika, watu walipendeza sana received_10207244597104832Kiti cha mfalme na malkia wake, Mr and Mrs Huckins, safi sana received_10207244596424815mapambo ya uwakika kabisa, viwango na ubora ulizingatiwa sana! received_10207244733868251-1…….Mama mama mamaaa  mama huyo mamaaa……. mama mzaa chema akifurahi kwa hisia zote binti kapata  mwenza, tena mzungu wa U.S.A aaah! Si utani ati ?? (just kidding). Hongera sana mama mzaa chema kwa kuozesha binti. Lakini ni kama lilivyo jina lake ni kwa neema tuu! received_10207244734388264-1Hahah! Safi sanaa! Hongereni mama na binti yake. received_10207269866136542 Nani kama MAMA?????!!!received_10207244733388239Siku kama hii ni vizuri kuwa na watu ambao kweli wanaumuhimu na wanakupenda kwa moyo wote. Harusi ni tukio la furaha na upendo hivyo ni vyema kujua wanao kuja kushuhudia ni watu watakao kuwa na furaha na upendo wa kweli nanyi nyote. received_10207244597544843Inaelekea shemeji yetu anapenda sana kuyarudi, natamani nijuwe kama ilikuwa ni ngoma za kilugha au za kikwao ??  received_10207244745188534 Wadada wa wazuri wenye nyuso za furaha na kupendeza sana. Mbarikiwe sana wapendwa   received_10207244593064731Once again, Congratulations Mr &Mrs Huckins. May the love of God dwell within you forever! ??

…....PLEASE DO NOT TAKE ANY PICTURE FROM THIS POST. THIS POST SHOULD ONLY BE SEEN IN THIS BLOG AND NOT SOMEWHERE ELSE. KINDLY RESPECT THIS FAMILY THEIR RIGHT TO PRIVACY.  THANKS

Leave a Reply