Father and son moment

IMG-20160130-WA0009Mtu na daddy yake. Huyu ni mdogo wangu anaitwa Isaka. Ni mtoto wa marehemu baba yangu mkubwa lakini amelelewa na kukulia kwetu toka akiwa na umri wa miaka mitano (5 yrs) mpaka sasa anakwenda 27. Kwahiyo hapa yupo na baba yake mlezi ambaye ni baba yangu mzazi. IMG-20160130-WA0007Huyu mdogo wangu ni mtaalam wa IT. Amesomea Nairobi, Kenya hivyo anafanya kazi Utegi Technical Enterprises Ltd. Yeye alizaliwa na matatizo ya kusikia na kuzungumza yani ni Bubu na pia ni Kiziwi. Na ndio maana tulimchukua kuishi naye ili apate elimu nzuri. Sasa jana baba alimkabidhi nyumba yake (ndio hii hapo juu ☝☝) ambayo ipo ndani la plot ya familia hapo Segerea. IMG-20160130-WA0006Ni nyumba iliyo kamilika yenye vyumba vitatu (3 bedrooms). Kijana kakuwa teyari kwa kujitegemea sasa. IMG-20160130-WA0008Hongera sana mdogo wangu Isaka kwa kupata nyumba nzuri sana. Asante baba kwa moyo wa upendo na ukarimu. Na sifa na utukufu zote zimwendee Mungu wa Mbinguni ??

4 thoughts on “Father and son moment”

  1. Hongera Sana Isaka. Hakika mkono unao toa ndio unaopokea zaidi. Mungu aendelee kubariki na kukuzidishia mjomba. Mimi umwita sir. Otieno Igogo sijaonaga kama yy ktk familia yetu sisiti kumtangaza mwenye heri au mbarikiwa wa mali na roho safi

  2. Amen,he is our DAD not father kwasababu dad hujua mipango yote mizuri kwa ajili ya familia yake,proud of you Dad and my boss Chief executive officer,mwenyezi mungu akupe maisha marefu daima na yenye baraka tele yeye ni wa pekee sana.

Leave a Reply